Polisi Uganda yatishia Waandishi | Matukio ya Afrika | DW | 16.05.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Polisi Uganda yatishia Waandishi

Polisi nchini Uganda imetishia kuwafungulia mashitaka mhariri na waandishi wawili wa gazeti la kibinafsi la Daily Monitor, kuhusiana na kuchapisha madai ya mwana wa rais Yoweri Museveni, kukirithi kiti cha baba yake

A line of Ugandan riot police is pictured as they clash with opposition supporters in the Namungoona suburb of Kampala, Uganda on January 24, 2012. Ugandan security personnel tried to detain opposition leader Kizza Besigye following a protest rally against rising living costs. AFP PHOTO/Michele Sibiloni (Photo credit should read MICHELE SIBILONI/AFP/Getty Images)

Polisi wa Uganda

Polisi nchini Uganda imetishia kuwafungulia mashitaka mhariri na waandishi wawili wa gazeti la kibinafsi la Daily Monitor, kuhusiana na barua iliyochapishwa na gazeti hilo juu ya kile kinachojulikana nchini Humo kama Mradi wa kumtayarisha mwana wa rais Yoweri Museveni, Brigedia Muhozi, kukirithi kiti cha baba yake. Barua hiyo iliandikwa na mkuu wa kitengo cha upelelezi cha Uganda Jeneral David Sejusa, akidai kuwa kuna mpango wa kuwauwa maafisa wanaoupinga mpango huo. Kuhojiwa kwa waandishi hao kumepingwa na wenzao nchini Uganda, ambao wanakuchukulia kama kitisho kwa uhuru wao. Kusikiliza zaidi kuhusiano na mkasa huo sikiliza mahojiano ya Daniel Gakuba na Ali Mutasa, mwandishi wa habari aliyeko nchini Uganda kwa kubonyeza alama ya kusikilizia masikioni hapo chini.

Mwandishi: Daniel Gakuba
Mhariri: Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada