1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Italia yafanya msako wa makundi ya kimafia

27 Julai 2013

Polisi Italia imefanya misako ya kupambana na makundi ya kimafia ambayo iliwalenga viongozi wakuu wa uhalifu wa kupangwa. Watu 51 ambao walisaidia kuongoza "vitendo haramu" mijini Rome na Ostia, walikamatwa.

https://p.dw.com/p/19F45
An unidentified person (C), one of the 51 people arrested for organised crime in Ostia, 30 km from Rome, is taken away by policemen at the Italian police Headquarter, in central Rome, on July 26, 2013. Italian police launched sweeping raids on Friday in a vast anti-mafia operation targeting around 100 people including top organised crime bosses accused of extortion, drug trafficking and murder. In "one of the largest operations ever carried out" in Rome, the blitz struck "a deadly blow to the mafia cell which had been operating in the capital for years," the police said. Amid accusations of drug trafficking, usury, extortion and control of the slot machine market, 51 people who helped lead "illegal activities" in Rome and the suburb of Ostia were served with arrest warrants, police spokesman Mario Viola told AFP. AFP PHOTO / ANDREAS SOLARO (Photo credit should read ANDREAS SOLARO/AFP/Getty Images)
Razzia gegen Mafia in Italien 26.07.2013Picha: Andreas Solaro/AFP/Getty Images

Polisi walisema waliokamatwa wanatuhumiwa kwa mauwaji, ulanguzi wa dawa za kulevya, unyang'anyi na udhibiti wa mashine za kuchezea kamari. Oparesheni ya pili iliwalenga wanachama wa genge la uhalifu la Ndrangheta katika mji wa Catanzaro katika eneo la kusini la Calabria. Katika eneo hilo polisi walikuwa na vibali vya kuwakamata karibu watu 50 hadi 70, ikiwa ni pamoja na wajasiriamali, wanasiasa na mawakili. Seneta mmoja wa chama cha aliyekuwa Waziri Mkuu Silvio Berlusconi cha siasa za wastani za mrengo wa kulia cha People of Freedom - PDL pia alifanyiwa uchunguzi kwa madai ya kununua kura kwa usaidizi wa makundi ya kimafia.

Karibu polisi 500 walishiriki katika uvamizi huo wa mjini Rome, pamoja na helikopta, vitengo vya mbwa wa kunusa na polisi wa majini, ambayo ililenga hasa kuwakamata majambazi wenye mafungamano na kundi la mafia la Sicilian ambao wamejaa katika mji huo mkuu wa Italia, kwa kununua mabaa na mikahawa kama maeneo ya kufanyia vitendo vyao vya kiuhalifu.

Mkuu wa kikosi cha polisi kilichoendesha operesheni hiyo Renato Cortese amesema magenge hayo ni hatari sana. Yanatumia silaha nzito, siyo tu kwa kufanya mauwaji, bali pia kuwahangaisha wakaazi wa Rome. Vibali hivyo vya kuwakamata vinatokana na uchunguzi wa muda mrefu wakati ambapo wapepelezi walifichua kila hatua ya uhalifu ndani ya kundi hilo la kimafia.

Raffaella D'Alterio, kiongozi mwanammke wa kundi moja la Mafia Italia baadaya kifo cha bwanake
Raffaella D'Alterio, kiongozi mwanammke wa kundi moja la Mafia Italia baadaya kifo cha bwanakePicha: picture-alliance/dpa

Chama cha kupambana na makundi ya kimafia, Libera, kimewapongeza polisi kwa upekuzi wao huo mjini Rome, kikionya kuwa magenge hayo hayajakita tu katika mji huo, bali pia yamekita mizizi katika kanda nzima.

Kando na makundi ya mafia, baadhi ya waliolengwa pia wanatuhumiwa kwa kutekeleza jukumu katika mauwaji kadhaa yaliyofanywa wakati wa vita vya umwagikaji damu baina ya makundi ya kimafia kati ya mwaka wa 2005 na 2011, pamoja na mamia ya vitendo vya unyang'anyi, ambapo walidai pesa za ulinzi kutoka kwa biashara.

‘Ndrangheta'---ambalo jina lake linatokana na neno la Kigiriki kumaanisha ujasiri na uaminifu--- lina mfumo imara wa ukoo ambao umefanya kuwa vigumu kupenya, na linashughulika na ulanguzi wa dawa za kulevya na silaha, ukahaba, unyang'anyi na ujenzi haramu.

Linazingatiwa na wengi kama kundi hatari na gumu kutabiri kuliko lile linalofahamika kama Cosa Nostra lenye makao yake Sicilian. ‘Ndrangheta' ni kundi linaloendesha uhalifu wa kimataifa kutoka kambi yake mjini Calabria na linahusishwa na opersheni kote magharibi na kaskazini mwa Ulaya ikiwa ni pamoja na Amerika na Australia.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri: Sekione Kitojo