Podolski ajiunga na Galatasaray | Michezo | DW | 06.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Podolski ajiunga na Galatasaray

Mshambuliaji wa Ujerumani Lukas Podolski amekamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Arsenal ya England na na kujiunga na Galatasaray ya Uturuki

Poldolski mwenye umri wa miaka 30 alikamilisha uhamisho wake siku ya Jumamosi baada ya kufanyiwa vipimo vya matibabu. Mjerumani huyo alisema uhamisho wake ulitokana na ujasiri na moyo wake.

Podolski alijiunga na timu ya Arsenal kutoka kilabu ya Ujerumani ya FC Koln mwaka 2012 kwa kitita cha pauni milioni 11 na kuweza kuifungia Arsenal mabao 31 kati ya mechi 82 alizochezea the Gunners.

Aliisaidia Arsenal kushinda kombe la FA mwaka 2013 lakini akaichezea kilabu ya Inter Milan msimu uliopita kwa mkopo.

Uwezo wake wa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika klabu ya Arsenal ulipungua baada ya mkufunzi Arsene Wenger kuwasajili wachezaji Mesut Ozil, Alexis Sanchez na Danny Welbeck.

Mwandishi: Bruce Amani/DW/DPA
Mhariri: Josephat Charo