1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pep: Man City watawaandalia Liverpool gwaride la heshima

Bruce Amani
29 Juni 2020

Wakati Bayern Munich wakisherehekea ubingwa wa Ujerumani, kuna jina la Mjerumani ambalo pia limepamba kurasa za magazeti na vyombo vya habari sio hapa tu bali pia Ungereza. Jurgen Klopp.

https://p.dw.com/p/3eW5I
Großbritannien Fußball | Manchester City | Pep Guardiola, Trainer
Picha: picture-alliance/dpa/M. Rickett

Ni mjerumani wa kwanza kuongoza klabu ya England kutwaa ubingwa. Liverpool walivunja kiu ya miaka 30 kwa kubeba taji la Premier League. Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema watawapa mabingwa hao wapya gwaride la heshima wakati timu hizo zitakutana dimbani Etihad Alhamisi wiki hii. "Tutawaandalia gwaride la heshima bila shaka. Tulijua hakika kuwa tutawapokea Liverpool katika njia nzuri zaidi wakati watakapokuja nyumbani kwetu. Hawawezi kulalamika na bila shaka tutafanya hilo kwa sababu wanastahili."

Klopp na vijana wake wamebaki na mechi saba huku wakiwa na pengo la pointi 23 kileleni. Huenda mbio za ubingwa wa zimeisha lakini bado kuna vuta nikuivzte katika nafasi za kandanda la Ulaya na kushushwa ngazi.

Washika mkia Norwich, nambari tatu kutoka mkiani Bournemouth na nambari nne kutoka mkiani West Ham wanahitaji kwa dhati pointi wakati wakipambana kuepuka kushushwa ngazi. Katika upande wa juu wa ligi, ni pointi sita tu zinazoitenganisha Leicester katika nafasi ya tatu kutoka kwa Manchester United katika nafasi ya sita.