1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis asema hatojiuzulu, afya yake ni nzuri

14 Machi 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis hana nia ya kujiuzulu kwani anahisi afya yake ni nzuri na anaweza kuendelea na majukumu yake.

https://p.dw.com/p/4dVOv
Papa Francis | Vatikan
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis Picha: Tiziana Fabi/AFP/Getty Images

Baba Mtakatifu ameyasema haya katika kitabu kipya ambacho dondoo zake zimechapishwa katika gazeti la nchini Italia la Corriere della Sera.

Katika kitabu hicho ambacho kinatarajiwa kutolewa rasmi mnamo Machi 19, papa anasema wazo la kujiuzulu ni ndoto kwa kuwa hana sababu yoyote ya kumpelekea kufanya hivyo.

Francis mwenye umri wa miaka 87, ameendelea kuwa dhaifu katika miaka ya hivi karibuni, ambapo amekuwa akitumia kiti cha magurudumu au mkongojo kutembea. Amekuwa pia akiugua mafua mara kwa mara jambo lililompelekea kupunguza maongezi yake mbele ya umma.