Pacquiao aondoa hofu kuhusu jeraha lake | Michezo | DW | 20.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Pacquiao aondoa hofu kuhusu jeraha lake

Manny Pacquiao leo amepuuzilia mbali shutuma kutoka promota wake Bob Arum baada ya shujaa huyo wa ndondi Mfilipino aliyejeruhiwa kukosa kwenda kumwona daktari kuhusiana na jeraha la bega

Pacman amesema aendelea kuliuguza jeraha hilo mwenyewe. Arum alimshambulia bondia wake huyo mwishoni mwa wiki akisema hana habari zozote kuhusu ni lini “Pacman” huenda akapanda tena ulingoni baada ya kuumia bega lake la kulia wakati wa pigano na Floyd Mayweather mwezi Mei.

Pacquaio amesema anamheshimu Arum maana yeye ni kama baba yake. Na anaamini kuwa promota huyo anaelezea tu wasiwasi wake kumhusu na hivyo anashukuru hilo na halichukulii kwa ubaya. Lakini hana sababu yoyote ya kuwa na hofu kuhusiana na jeraha lake maana anaendelea kupata nafuu haraka sana kuliko ilivyotarajiwa.

Na kufikia hapo ndipo nakamilisha michezo kwa sasa kwa mengi zaidi, tembelea ukurasa wetu wa michezo, fungua dw.com/Kiswahili, na pia unaweza kuwasiliana nami kupitia facebook na Twitter mimi ni Bruce Amani. Kwaheri

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/APE/DPA/Reuters
Mhariri:Josephat Charo