Olmert apoteza mshiriki wake Lieberman | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.01.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Olmert apoteza mshiriki wake Lieberman

Waisraeli na Wapalestina wameendelea na mazungumzo ya amani leo lakini hali kwa ujumla katika eneo hili ni kinyume na ishara za amani.

Avigdor Lieberman

Avigdor Lieberman


Raia watatu wa Kipalestina waliuawa katika shambulizi la anga la Israeli katika eneo la ukanda wa Gaza. Wakati huo huo chama cha Mrengo wa kulia cha Israel kimejitoa katika serikali ya muungano chini ya waziri Mkuu Ehud Olmert, baada ya kukasirishwa na kuanza kwa majadiliano ya amani na Palestina.


Jeshi la Israeli lilikiri kuwa liliwashambulia kwa makosa Wapalestina watatu raia wa kawaida wakiwa ndani ya gari lililo karibu na lengo lao la kijeshi, yaani gari na msaidizi wa Hamas anayetengeneza mabomu. Wapalestina wengine kadhaa walijeruhiwa katika mashambulizi mengi ya anga. Mapigano kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Hamas yalizusha tena baada ya kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani hapo Novemba. Karibu kila siku, jeshi la Israel linalishambulia eneo la Gaza katika juhudi za kusimamisha vamio katika eneo la Kusini kwa Israel. Katika eneo la Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan, jeshi la Israel limemua kiongozi wa kundi la Islamiv Djihad. Jana tu, Wapalestina 19 waliuawa katika mapigano haya, miongoni wao alikuwa mtoto wa kiongozi mmoja wa kundi la Hamas.


Wakati huo huo, wajumbe wa Israel na Wapalestina walikutana tena kuendelea na mazungumzo ya amani kuhusu masuala magumu. Lakini serikali ya muungano ya Ehud Olmert ya Israel inazidi kupotea ungwaji mkono baada ya chama ya mrengo wa kulia cha Israel Beitenu kilijitoa katika serikali hiyo.


Alipozungumza na waandishi wa habari leo mjini Yerusalem, kiongozi wa chama hiki, Bw. Avigdor Liebermann alisema alimfahamisha waziri mkuu Olmert leo asubuhi kuhusu hatua hiyo. Sababu ni mazungumzo ya amani na upande wa Palestina yaliyoanzishwa hivi karibuni. Lieberman alisema: "Ni wazi kabisa kwa wote kwamba majadiliano haya hayatakuwa na matokeo yoyote, na ikiwa ni hivyo suali ni: Kwa nini tunajitoa katika serikali ya muungano? Mimi nataka kusisitiza kwamba mazungumzo yoyote kuhusu suala la ardhi ni kosa kubwa. Kwa maoni yangu ni kosa kubwa ambalo halielekewi kabisa."


Hatua hiyo ilitarajiwa itachukuliwa. Tayari kabla ya mkutano wa kilele wa Annapolis, Marekani hapo Disemba, Bw. Liebermann aliarifu kuwa atajitoa katika serikali ya Ehud Olmert ikiwa yeye atajadili na rais wa mamlaka ya Kipalestina Abbas kuhusu masuala ya Yerusalem, wakimbizi na mipaka. Serikali ya muungano ya Ehud Olmert sasa imepoteza viti 11 bungeni. Lakini inabakia na viti 67 ambavyo ni uwingi katika bunge hili la Knesset lenye viti 120 kwa ujumla.


Chama kingine katika muungano huu cha msimamo mkali wa Orthodox, Shas, chenye viti 12 kimesema pia kitajitoa pindi suala la kugawa mji wa Yerusalem litajadiliwa.


Juu ya hayo Olmert anatarajiwa kukabiliwa na changamoto kubwa zaidi baadaye mwezi huu pale ripoti kuhusu makosa ya Israel katika viti dhidi ya Lebanon itakapotolewa. 

 • Tarehe 16.01.2008
 • Mwandishi Dreyer, Maja
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CqwI
 • Tarehe 16.01.2008
 • Mwandishi Dreyer, Maja
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CqwI

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com