1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obasanjo ajaribu kupatanisha Côte d'Ivoire

Oumilkher Hamidou10 Januari 2011

Obasanjo haondowi uwezekano wa kutumiwa jeshi kumng'owa madarakani Gbagbo.

https://p.dw.com/p/zvly
Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun ObasanjoPicha: AP


Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo jana alikuwepo nchini Côte d'Ivoire katika jitihada za kuutatua mzozo wa kisiasa kati ya Rais Laurent Gbagbo na mpinzani wake Alassane Ouattara anayetambuliwa kimataifa.

Duru za karibu na na Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS, zimeeleza kuwa Obasanjo alikuwa nchini Côte d'Ivoire kwa ajili ya mazungumzo. ECOWAS imekuwa ikijaribu kuutatua mzozo huo wa kisiasa.

Mwanadiplomasia mmoja wa Afrika ameliambia shirika la habari la AFP, kuwa Obasanjo aliwasili Abidjan siku ya Jumamosi na siku ya Jumapili alifanya mazungumzo na Gbagbo pamoja na Ouattara.

Kwa mujibu wa duru hizo, Obasanjo ametumwa na mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS, Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan. Ziara hiyo ya Obasanjo ilikuwa haijatangazwa.