NOUAKCHOTT:Serikali yaomba msaada kukarabati mji uliozama | Habari za Ulimwengu | DW | 12.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NOUAKCHOTT:Serikali yaomba msaada kukarabati mji uliozama

Mauritania inatoa wito wa msaada kutoka kwa jamii ya kimataifa ili kukarabati upya mji uliozama kufuatia mafuriko wiki iliyopita.Yapata nusu ya wakazi wote nchini humo walipoteza makazi yao katika mafuriko.Waziri wa Fedha Abderrahmane Ould Hemma Vezzaz aliwaeleza wafadhili wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Milki za Kiarabu vileve Umoja wa Mataifa kuwa serikali yake inatarajia kuchanga dola milioni 4 ili kukarabati mji wa Tnitane ulio kusini mashariki mwa nchi.

Yapata nusu ya wakazi wote alfu 60 wa mji huo wameathiriwa na mafuriko yaliyotokea siku ya jumanne iliyopita na kusababisha vifo vya watu 2.Kulingana na kiongozi huyo takriban familia alfu 2500 wanajumuishwa katika mpango wa kuwajengea makazi mapya na fedha hizo zitawawezesha kujenga nyumba zao katika maeneo ya juu zaidi,kuweka mabomba ya maji vilevile kusambaza huduma za umeme,kujenga barabara na shule.

Nchi ya Libya ilipeleka ndege mbili zilizosheheni vifaa vya matumizi pamoja na hema na mablanketi yatakayotumiwa na wahanga wa mafuriko.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com