Nkunda atoa changamoto | Habari za Ulimwengu | DW | 02.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Nkunda atoa changamoto

NAIROBI:

Jamadari-muasi Laurent Nkunda,katika mahojiano,ameeleza kwamba kuna hali ya vita iliozuka baina vikosi vyake na vile vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo-huko mashariki mwa nchi hiyo.Jamadari nkunda ameiambia idhaa ya B BC kwamba jeshi la J.K.Kongo liliungwamkono na wahutu katika kulihujumu jeshi lake huko Kivu.Kwahivyo, alisema hataitikia amri yoyote ya kuvipokonya silaha vikosi vyake.

Jamadari nkunda alisema zaidi kwamba vikosi vyake viliwakabidhi waasi wa kihutu wa Rwanda wa FDLR kwa vikosi vya kuweka amani vya UM nchini Kongo,lakini serikali ya kongo na Wahutu walivigeukia vikosi vyake
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com