Nigerian violence.
29 Julai 2009Matangazo
ABUJA.
Rais Umaru Yar'Adua wa Nigeria amesema majeshi ya usalama yatawasaka na kuwazima waasi waliobakia, wa kundi la waislamu waliosababisha mapigano ambapo watu wasiopungua 150 waliuawa katika siku tatu zilizopita nchini Nigeria.
Ghasia zilizuka mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya baadhi ya waumini wa kundi linalojiita Boko Haram kukamatwa katika jimbo la Bauchi kaskazini mwa Nigeria.
Kundi hilo linaloiga mfano wa taliban linapigania kupitishwa na kuenezwa kwa sheria za kiislamu ambazo tayari zinatumika katika miji 12 ya kaskazini mwa Nigeria.
Mwaka jana watu 700 waliuawa katika mji wa Jos, kutokana na mapambano baina ya waislamu na wakristo.