Nia ya kusaidia Wakurdi yaoneshwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Nia ya kusaidia Wakurdi yaoneshwa

Siku 6 baada ya Marekani kurudi tena Iraq na kuanza mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la kisunni linalojiita dola la kiislamu Ufaransa nayo imeanza kupeleka silaha wakati nchi nyingine za Ulaya zikionesha nia hiyo

Wachambuzi wanasema kuwaangamiza wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita dola la kiislam kutachochea propaganda zinazo wavutia mamia ya vijana wanaotaka kujiunga na kundi hilo kutoka barani ulaya. Kamishna wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binaadamu Navi Pillay alilitaja suala hilo kama ukiukwaji wa dhamiri ya kibinaadamu usiovumilika.

Katika mazungumzo yake ya May 2013, Pillay alisema wachunguzi wa umoja wa mataiafa walipata ushahidi mkubwa wa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadam nchini Syria ambao umekuwa unahusishwa na rais Bashar al-Assad.

Idadi kubwa ya watu yapoteza maisha

Irak Flüchtlinge in Erbil 13.08.2014

Wakimbizi wa Iraq katika eneo la Erbil

Na sasa, mbali ya ukweli kwamba zaidi ya watu 120,000 tayari wamepoteza maisha wito huo ulishindwa kuyashawishi mataifa ya magharibi yenye uwoga wa kutumia nguvu,kuingia kijeshi nchini humo.

Mwaka mmoja baadae mataifa yenye nguvu ya magharibi yanaonesha kwa uchache nia ya kushiriki kwao Iraq.

Jumatano wiki hii rais Francois Hollande alisema nchi yake itawasaidia wapiganaji wa Kikurdi katika eneo la Kurdistan kaskazini ya Iraq kupambana na kundi la IS. Nao maofisa wa serikali wamekataa kufichua kuhusu aina ya silaha wanazozitumia kundi hilo , Lakini waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema silaha hizo ni za kisasa.

Hoja hiyo ilionekana kuzishawishi nchi nyingine za Ulaya ikiwa ni pamoja na Uingereza ambayo ilikuwa mshirika mkuu wa Marekani wakati wa uvamizi wa Marekani nchini Iraq katika mwaka wa 2003.

Jitihada za Uingereza

Mpaka sasa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameelekeza juhudi zake katika kutoa misaada kwa wakimbizi waliokwama milimani lakini anakumbwa na shinikizo la kutakiwa kuchukua hatua zaidi.

Ufaransa, ambayo ilikataa kujiunga katika operesheni ya mwaka wa 2003, haijatwikwa jukumu lolote kuhusiana na hali ya sasa Iraq. Lakini picha zinazowaonyesha maelfu ya wakristo walio wachache na watu wa jamii ya Wayazidi wanaojaribu kuepuka vitisho vya IS kuwataka wajiunge na dini ya Kiislamu, au wauliwe, zimeigusa mioyo ya taifa hilo ambalo limekita mizizi ya Kikatoliki, licha ya kuwa na taasisi zisizofungamana na dini.

Wakiandika katika gazeti la Le Monde, mawaziri wakuu watatu wa zamani wa Ufaransa wamemwambia Hollande kuwa bara la Ulaya lina "jukumu la kuwalinda Wakristo katika Mashariki ya Kati".

Ufaransa inajiandaa kwa kitisho cha kurejea kwa takribani raia wake 900 waliopewa mafunzo ya itikadi kali na ambao wamekuwa wakipigana sambamba na makundi ya nchini na Syria, Iraq na Libya, na inatarajia kukabiliana na hali hiyo kabla warejee nyumbani.

huku jeshi la Iraq likiwa katika mparanganyiko, majeshi ya Kikurdi yaliyopewa mafunzo ya hali ya juu yanatoa matumaini ya kupambana na kulishinda kundi la IS ambalo liliutwaa mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq wa Mosul na miji mingine ya kaskazini mwa nchi hiyo bila upinzani wowote.

Kirk Sowel, mchambuzi wa masuala ya siasa za Iraq anasema mvuto wa IS kwa kiwango kikubwa unatokana na mafanikio yake, hali inayoonekana kutoepukika. Anaongeza kuwa kwa kuwapa silaha wapiganaji wenye misimamo huru kama vile wa Kikurdi hakuwezi kukosa athari zake.

Kama Wakurdi wataliangamiza kundi la IS, na kisha serikali ya Baghdad iendelee kuporomoka na kujikuta katika hali ya kutofuata sheria kuna uwezekano mkubwa kuwa jeshi la Kikurdi linaweza kujaribu kujiimarisha dhidi ya serikali ya Baghdad kwa kuinyima mapato yanayotokana na mafuta.

Mwandishi: Mwazarau Mathola/DPA

Mhariri: Yusuf Saumu

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com