1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni rasmi, Timo Werner atatua Chelsea Julai

18 Juni 2020

Klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya England Chelsea imethibitisha kufikia makubaliano na RB Leipzig ya Ujerumani kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wao Timo Werner.

https://p.dw.com/p/3dyHz
Fußball Bundesliga RB Leipzig vs 1.FC Köln Tor Werner 1:0
Picha: AFP/O. Andersen

Kwa mujibu wa tovuti ya Chelsea, Werner ambaye ni raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24 atajiunga na miamba hao wa London mwezi Julai, pale msimu wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga utakapokamilika. "Nina furaha sana kujiunga na Chelsea, ni fahari kujiunga na timu hii," alisema Werner. "Natumai nitakuwa na msimu ujao wenye mafanikio na wachezaji wenzangu wapya, meneja wangu mpya na bila shaka mashabiki wa Chelsea," aliongeza Werner. Mshambuliaji huyo amefunga magoli 32 katika mechi 43 katika klabu ya RB Leipzig msimu huu na katika timu ya taifa ya Ujerumani, amecheka na wavu mara 11 katika mechi 29.