Ni nini unaweza kufanyia hizo fedha? | Mada zote | DW | 18.08.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ni nini unaweza kufanyia hizo fedha?

Msimu wa soka 2017/18 umeanza. Kwa mashabiki wengi, kipindi kirefu cha njaa kimefikia mwisho, lakini kwa vilabu vingi, kengele za fedha zinaanza kulia. Hakujawahi kuwa na fedha nyingi katika soka kama ilivyo sasa.

Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Paul Pogba: Wote walisajiliwa kwa fedha nyingi au takriban euro milioni 100 kila mmoja kama ada ya uhamisho. Wengi wamesema kuwa hilo halikubaliki. Lakini ghafla hali imefikia kiwango tofauti kutokana na kiasi cha fedha ambacho Neymar alinunuliwa. Kwa sasa hakika hata Bundesliga itahisi athari zake.