Nguli wa ragbi Jonah Lomu afariki dunia | Michezo | DW | 18.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Nguli wa ragbi Jonah Lomu afariki dunia

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya New Zealand ya mchezo wa rugby Jonah Lomu ameaga dunia. Lomu aliyekuwa na umri wa miaka 40 amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo

Salamu za rambirambi zinaendelea kutolewa kutoka wa wanamichezo na jamaa na marifiki kila pembe duniani kufuatia kifo chake.

Lomu alifanyiwa ubadilishwaji wa figo yake, ambayo ilikua ikimsumbua, mwaka 2004 na iliyopelekea yeye kustaafu kucheza mchezo wa raga. Mchezaji huyo aliogopwa sana na wapinzani kutokana na nguvu zake na aliichezea timu ya taifa ya All Blacks michezo 73 kuanzia mwaka 1994 mpaka 2002 na kufunga mabao 43. Lomu anachukuliwa mmoja wa wachezaji maarufu zaidi wa mchezo huo ulimwenguni

Alifariki ghafla baada ya kurejea kutoka Uingereza ambako kando na kuupigia debe mchezo wa ragbi, aliishangilia timu yake ya taifa ambayo ndiyo iliyobeba Kombe la Dunia la Ragbi lililomalizika majuzi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdulrahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com