Neid kujiuzulu kama kocha wa timu ya wanawake ya Ujerumani | Michezo | DW | 30.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Neid kujiuzulu kama kocha wa timu ya wanawake ya Ujerumani

Silvia Neid atajiuzulu kama kocha wa timu ya Ujerumani ya wanawake katika mwaka wa 2016. Shirika la Kandanda la Ujerumani limesema nafasi ya Neid itachukuliwa na aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa Steffi Jones

Chini ya ukufunzi wa Neid, Ujerumani ilibeba Kombe la Dunia la mwaka wa 2007 na ikashinda taji la Ubingwa wa Ulaya mwaka wa 2009 na 2013.

Wajerumani hao ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kushinda Kombe la Dunia mwaka huu nchini Canada, litakaloanza Juni 6 hadi Julai 5 wakiongozwa na Neid.

Neid, mwenye umri wa miaka 50, kisha atachukua wadhifa mpya kuanzia Septemba 2016, ulioundwa na shirikisho la kandanda Ujerumani – DFB wa kitengo cha kutafuta vipaji vipya.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com