NEC kutoa matokeo ndani ya masaa 72 | Tanzania Yaamua 2015 | DW | 30.09.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Tanzania Yaamua 2015

NEC kutoa matokeo ndani ya masaa 72

Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imerejea msimamo wake wa kuhisabiwa kura zote zitakazopigwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwenye vituo vya kupigia kura, hatua iliyopokewa vyema na wadau wa uchaguzi.

default

Pirikapirika za kuelekea uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba zinazidi kushika kasi. Taarifa ya NEC iliyosema ni ya kusimamia haki katika mchakato huo inasema kwa sasa kura zote kuanzia udiwani, ubunge na Urais zitahesabiwa katika vituo vya kupiga kura na matokeo yake kutolewa hapo hapo katika kipindi kisichozidi masaa 72.

Sudi Mnette anazungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Rutaraka Ate Junior, juu ya kauli hii ya NEC na maana yake kwa uchaguzi wa mwaka huu unaotajwa kuwa wa kihistoria.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com