NAPLES Msitumie jina ka Mungu kuua asema Baba Mtakatifu | Habari za Ulimwengu | DW | 22.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAPLES Msitumie jina ka Mungu kuua asema Baba Mtakatifu

Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 amesema jina la Mungu lisitumiwe kuhalalisha matumizi ya nguvu.

Baba Mtakafitu ametoa mwito huo kwa viongozi wa dini zote wanaohudhuria mkutano wa siku tatu katika mji wa Neaple nchini Italia.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki ameonya dhidi ya dini kutumiwa kama vyombo vya chuki

Ameahidi kuwa kanisa katoliki litaendelea kufanya mazungumzo ili kujenga mawasiliano baina ya tamaduni.

Lakini askofu mkuu wa Canterburry Rowan Williams amesema mkutano huo unafanyika katika mazingira ya mgawanyiko mkubwa kuliko ilivyokuwa miaka 21 iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com