Nani atamaliza kwenye nne bora England? | Michezo | DW | 15.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Nani atamaliza kwenye nne bora England?

Kivumbi cha kuwania kumaliza msimu katika nafasi nne bora nchini England kinapamba moto huku Tottenham Hotspur, Chelsea, Manchester United na Arsenal wote wakiwania nafasi mbili zilizoko.

Spurs ni wa tatu baada ya kuwacharaza Huddersfield mabao 4-0 ambapo nahodha wa Kenya Victor Wanyama aliweza kuwa miongoni mwa waliotikisa wavu kwenye mechi hiyo.

Chelsea baada ya kufungwa na Liverpool wanasalia kwenye nafasi ya nne ingawa wanaweza kuondolewa na katika nafasi hiyo na Manchester United ambao hawajacheza mechi moja, United wao waliponea nyumbani kwao kwa kupata ushindi wa mbili moja dhidi ya West Ham ambapo Paul Pogba alipachika wavuni mikwaju miwili ya penalti.

Arsenal wanaingia uwanjani usiku wa leo na iwapo watatoa ushindi dhidi ya Watford huko Vicarage Road basi watakwea hadi katika nafasi ya nne kwa kuwa wamewazidi Chelsea kimabao.