1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stuttgart: Serhou Guirassy hana nia ya kuondoka

24 Desemba 2023

Mwenyekiti wa klabu ya VfB Stuttgart Alexander Wehrle anaamini kuwa mfungaji wao bora Serhou Guirassy hataondoka klabuni humo mwezi Januari.

https://p.dw.com/p/4aXq9
 VfB Stuttgart vs. SV Darmstadt 98 |  Serhou Guirassy
Mshambuliaji wa VfB Stuttgart Serhou GuirassyPicha: Wolfgang Frank/Eibner/IMAGO

Mwenyekiti wa klabu ya VfB Stuttgart Alexander Wehrle ameliambia gazeti la Ujerumani la The Bild am Sonntag kwamba haoni dalili za mshambuliaji huyo kuondoka Stuttgart.

Guirassy amefunga mabao 17 msimu huu ambayo yameisaidia klabu hiyo kushikilia nafasi ya tatu kwenye jedwali la ligi kuu ya Bundesliga, baada ya kuepuka shoka la kushushwa daraja msimu uliopita kupitia mechi ya mchujo.

Wehrle amemmiminia sifa kocha Sebastian Hoeneß kwa kuwanoa vizuri wachezaji japo ametahadharisha juu ya kupunguza kasi ya mchezo kuelekea mechi za mzunguko wa pili.

Soma pia: Tuchel: Hatukujiandaa vizuri dhidi ya Frankfurt

Lengo la Stuttgart kwa wakati huu ni kukusanya alama 40 haraka iwezekanavyo, ambazo zinahitajika ili kuzuia timu kushushwa daraja. Klabu hiyo ina alama 34 baada ya kucheza 16 msimu huu.

Ligi ya Bundesliga iko kwenye mapumziko mafupi ya Krismasi na sherehe za mwaka mpya na itarindima tena mnamo Januari 12 mwaka 2024 wakati Bayern Munich wakiialika nyumbani Allianz Arena TSG Hoffenheim.