1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi habari wa Congo aachiwa huru kwa muda

Iddi Ssessanga
13 Oktoba 2021

Mwandishi habari aliekamatwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Septemba kwa kumiliki vidio inayoonesha mauaji ya wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017, amepewa dhamana Jumanne akisubiri uchunguzi zaidi.

https://p.dw.com/p/41cOe
Deutschland Jamaika-Koalition Sondierungsgespräche | Symbolbild Medien
Picha: Reuters/A. Schmidt

Mwandishi huyo Sosthene Kambidi, anaeufanyia kazi mtandao wa habari wa Actualite.cf na wakati mwingine mashirika ya habari ya kimataifa, alikamatwa wiki tatu zilizopita na kuambiwa anachunguzwa kwa kula njama ya uhalifu, uasi na ugaidi, lakini waendesha mashtaka hawakutoa ufafanuzi zaidi.

Kambidi alichangia kwenye uchunguzi wa kituo cha Redio France International na shirika la Reuters mwezi Desemba 2017, ambao ulifuchua kwamba maafisa wa idara ya usalama ya serikali, walisaidia kupanga safari ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuchunguza ripoti za ukatili katika mkoa Kasai nchini Congo.

Waendesha mashtaka wameachana na uchunguzi wa kula njama, uasi na ugaidi, lakini wanaendelea kuchunguza namna Kambidi alivyoshindwa kutekeleza jambo linalotakiwa.

Msemaji wa jeshi aligoma kuzungumzia kesi hii na mwwendesha mashtaka mkuu wa jeshi hakupatikana kutoa kauli.