1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanasoka wa zamani wa Ujerumani Gerd Mueller amefariki

16 Agosti 2021

Mshambuliaji mashuhuri wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Gerd Mueller alifariki jana akiwa na umri wa miaka 75.

https://p.dw.com/p/3z28Z
Deutschland | Fußball-Legende Gerd Müller im Alter von 75 Jahren gestorben
Picha: Popperfoto/Getty Images

Mshambuliaji mashuhuri wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Gerd Mueller alifariki jana akiwa na umri wa miaka 75. Taarifa hizi zimethibitishwa na klabu yake ya zamani ya Bayern Munich.

Rais wa klabu hiyo Herbert Heiner alisema ni siku ya huzuni kwao na kumtaja Mueller kuwa ni mshambuliaji bora kabisa kuwahi kutokea katika klabu hiyo.

Enzi ambazo alikuwa akiwika miaka ya 1960 na 1970, Mueller aliweka rekodi ya kuifungia timu yake ya Bayern katika ligi ya Ujerumani mabao 365, pamoja na kuifungia timu ya taifa ya iliyokuwa Ujerumani Magharibi mara 68 katika mechi 62 za kimataifa.