Mwanamke raia wa Cote d′voire akamatwa na Cocaine tumboni | Matukio ya Afrika | DW | 29.12.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mwanamke raia wa Cote d'voire akamatwa na Cocaine tumboni

Raia wa Cote d'voire akamatwa Thailand baada ya mashine ya uchunguzi kugundua kilo 1.2 za cocaine tumboni mwake

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 27 raia wa Cote d'voire, amekamatwa katika kisiwa cha Phuket nchini Thailand baada ya mashine ya uchunguzi kwenye uwanja wa ndege, kugundua zaidi ya kilo moja ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine tumboni mwa mwanamke huyo, zilizokuwa zimefungwa kwenye pakiti ndogondogo.

Mwanamke huyo alisimamishwa na maafisa jana jioni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Phuket baada ya kutua akitokea Doha. Taarifa zilizotolewa na mkuu wa ofisi ya bodi ya kupambana na dawa za kulevya nchini Thailand zimesema mashine hiyo ya uchunguzi iligundua pakiti ndogondogo zaidi ya 60 kwenye tumbo lake, zilizojazwa kiasi ya kilo 1.2 za Cocaine, zinazodhaniwa kuwa zilikuwa zinapelekwa kwa wafanyabiashara matajiri katika mji wa Bangkok.