Mvua kubwa zanyesha visiwani Comoro | Matukio ya Afrika | DW | 27.04.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mvua kubwa zanyesha visiwani Comoro

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika visiwa vya Comoro kwa karibu wiki nzima, zimesababisha uharibifu mkubwa ikiwa ni pamoja na miundo mbinu.

Kisiwa cha Comoro kilichokumbwa na mvua kubwa

Kisiwa cha Comoro kilichokumbwa na mvua kubwa

Pia visima vya kuhifadhia mafuta vimeingia maji na kusababisha uhaba wa mafuta na matatizo ya usafiri. Maafisa wanasema zaidi ya watu 11,000 wamepoteza takriban kila kitu .huku hali ikitajwa kuwa mbaya zaidi katika kisiwa kidogo cha Moheli ambako baadhi ya vijiji vimezungukwa na maji.

Mohamed Abdulrahman mezungumza na waziri wa ndani wa visiwa hivyo Ahmed Abdullah na kwanza anasimulia juu ya hali ilivyo wakati huu.

(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mahojiano: Mohammed Abdul-Rahman/Waziri Ahmed Abdullah

Mhariri: Mohammed Khelef

Sauti na Vidio Kuhusu Mada