Mutharika amfuta kazi waziri wa kilimo kwa ufisadi | Matukio ya Afrika | DW | 22.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Mutharika amfuta kazi waziri wa kilimo kwa ufisadi

Rais Peter Mutharika wa Malawi amemfukuza kazi waziri wake wa kilimo kufuatia uchunguzi uliofanyika juu ya ufisadi kwenye manunuzi ya mahindi katika wakati taifa hilo likikabiliwa na njaa.

George Chaponda ameondoshwa kwenye wadhifa wake kwa kubainika kuzidisha gharama za manunuzi ya mahindi kutoka Zambia.

Jumla ya dola milioni 34.5 zimetumika na taifa hilo la kusini mwa Afrika, ambalo linakabiliwa na kitisho cha njaa kama yalivyo maeneo kadhaa ya eneo hilo, lakini imefahamika kuwa mamilioni ya fedha hizo yalihifadhiwa nyumbani kwa Chaponda.

"Rais amemuondoa Chaponda kama waziri wa kilimo mara moja baada ya kugundulika akiwa na mamilioni ya fedha nyumbani kwake jana," Waziri wa Habari Nicolaus Saudi ameliambia shirika la habari la Reuters leo (22 Februari).

Mwezi uliopita, Rais Mutharika alikuwa ameagiza uliopita uchunguzi kuhusina na manunuzi hayo.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com