Murray alenga kusalia kileleni katika tennis | Michezo | DW | 21.11.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Murray alenga kusalia kileleni katika tennis

Andy Murray amemwonya Novak Djokovic kuwa yuko tayari kuendeleza udhibiti wake kileleni mwa mchezo wa tennis baada ya Mscotland huyo alikamilisha msimu wake katika nafasi ya kwanza ulimwenguni

Murray alionyesha mchezo wa kusisimua na kumpiku Djokovic 6-3, 6-4 na kushinda taji la dunia la ATP Tour Finals katika uwanja wa O2 Arena mjini London hapo jana.

Baada ya kumaliza muda mwingi wa taaluma yake akiwa kwenye kivuli cha mafanikio makubwa ya wanatenis maarufu kama Djokovic, Roger Federer na Rafael Nadal, Murray mwenye umri wa miaka 29 sasa anaweza kujigamba kuwa mchezaji bora duniani na hana nia yoyote ya kuachia usukani bila kupigania hadhi hiyo.

"ningependa kujaribu na kubakia pale, bila shaka. Imekuwa juhudi kubwa katika miezi mitano, sita iliyopita ili kufikia pale,” alisema Murray baada ya ushindi huo wake wa 24 mfululizo kumpa taji la tano katika mashindano yake matano yaliyopita.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef