1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muda wa ujumbe wa uangalizi Syria wamalizika

17 Agosti 2012

Umoja wa mataifa unaondoa ujumbe wake nchini Syria kutokana na kuongezeka kwa machafuko nchini humo. Baraza la usalama la umoja wa mataifa limefikia uamuzi huo jana(16.08.2012).

https://p.dw.com/p/15rb8
epa03253025 UN observers are seen ahead of their daily patrols of restive cities at the Dama Rose hotel in Damascus, Syria, 07 June 2012. According to media reports on 07 June 2012, the Syrian army and civilians prevented UN observers from inspecting the site of a reported massacre in the central province of Hama, the head of the UN mission in the country confirmed. EPA/YOUSSEF BADAWI
wachunguzi wa umoja wa mataifa mjini DamascusPicha: picture-alliance/dpa

Pamoja na hayo umoja wa mataifa ulimtangaza rasmi Lakhdar Brahimi kuwa mwanadiplomasia atakayeshughulikia mzozo wa Syria akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Kofi Annan. Masharti ya utendaji wake wa kazi hata hivyo yanaendelea kuwa magumu.

Urusi ilipendelea sana, ujumbe huo wa uchunguzi urefushiwe muda wake kwa mara nyingine, hatimaye lakini mwishowe ilikubali kushindwa. Azimio la Urusi halikuweza kupata muungaji mkono katika baraza la usalama. Balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa Vitali Churkin hakuweza kulizuwia kundi kubwa la wajumbe wa baraza la usalama, kwa kuwa nchi hizi hazijaonyesha hatua ya kuweza kumaliza machafuko na pia suluhisho la kisiasa nchini Syria.

"Wajumbe wa nchi hizi hawaonyeshi ishara ya kumaliza machafuko, na kufanyakazi kwa ajili ya kuleta suluhisho nchini Syria".

Lakhdar Brahimi, Special Advisor on Iraq to the Secretary-General speaks to the media after a meeting with Kofi Annan, the UN Secretary-General and the Group of Friends of Iraq. The U.N. judgment on elections throws open the debate over how to transfer sovereignty and end the U.S. occupation _ though not the U.S. military presence _ among the Americans, Iraq's Governing Council and powerful Shiite clerics, who derailed American plans by demanding an early election. (AP Photo/Osamu Honda)
Mwanadiplomasia kutoka Algeria Lakhdar BrahimiPicha: AP

Hapo kabla balozi wa Ufaransa katika umoja wa mataifa Gerard Araud akiwa kama rais wa baraza la usalama alitangaza kufikishwa mwisho rasmi kwa ujumbe huo wa uchunguzi. Kwa upande mwingine, Araud amesema madhumuni ya kuwapo kwa ujumbe huo hayakufikiwa. Utawala wa Syria pia haukuacha matumizi ya silaha nzito, na machafuko hayajapungua. Mamlaka ya ujumbe huo ambayo yalirefushwa mwezi mmoja uliopita, yanamalizika usiku wa manane siku ya Jumapili. Ilikuwa mwezi Aprili katika baraza la usalama ambapo ujumbe huo ulipewa jukumu la kuzuwia mapigano nchini Syria, lakini jukumu hilo halikutimia, na tangu katikati ya mwezi Juni ujumbe huo umekuwa kwa kiasi kikubwa katika hoteli waliyofikia. Umoja wa mataifa unapaswa kuwapo nchini Syria, lakini kama alivyopendekeza katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-moon, hata kama ujumbe huo utaondolewa, lakini ni lazima usaidizi uendelee.

"Tunakubaliana na pendekezo lake la kuanzisha ofisi ya uratibu mjini Damascus".

Anasema hivyo Araud baada ya kikao kilichochukua karibu saa mbili. Utaratibu wa kuwa na uwakilishi mpya wa umoja wa mataifa nchini Syria , utakao kuwa na watu kati ya 20 na 30 , utapata msaada pia kutoka Ujerumani. Kwa mujibu wa mwakilishi wa Ujerumani katika umoja wa mataifa Miguel Berger, ofisi hiyo ya uratibu mbali ya kuwa na watu wa kutosha lakini pia wenye ujuzi unaostahili, ili kuweza kuangalia haki za binadamu.

French United Nations Ambassador Gerard Araud speaks after a Security Council meeting regarding the situation in Libya Thursday, March 24, 2011 at United Nations headquarters in New York. (AP Photo/Stephen Chernin)
Rais wa baraza la usalama Gerard AraudPicha: AP

"Tunaunga mkono , kwa kuwa ni muhimu kuwapo na ushirikiano wa kisiasa , uangalizi wa haki za binadamu, utoaji misaada ya kiutu na ndio sababu kuwapo kwa umoja wa mataifa ni muhimu sana".

Ndio sababu kulikuwa na mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka mataifa matano yenye kura ya veto katika umoja wa mataifa , China, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Marekani, pamoja na wawakilishi kutoka Uturuki, Iraq, Kuwait na Qatar. Mkutano huo wakati huo ulikuwa na lengo la kuunda serikali ya mpito.

Mwandishi: Schmidt, Thomas / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri:Josephat Charo