Mtoto wa kike ahitimu shule | Noa Bongo | DW | 20.04.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Noa Bongo

Mtoto wa kike ahitimu shule

Kutojua kusoma na kuandika ni jambo ambalo linaweza kukuaibisha na linayaathiri maendeleo ya mtu binafsi.Hilo ndilo wanalolitambua ndugu wawili Latifa na Elinam katika makala haya mapya ya Noa Bongo-Jenga Maisha Yako.

Msichana akiwa shuleni

Msichana akiwa shuleni

Kujua kusoma na kuandika pamoja na elimu ni mambo muhimu yanayokubalika kuwa chachu ya maendeleo. Hata hivyo, kiasi cha zaidi ya watu wazima milioni 150 kote ulimwenguni hawawezi kusoma na kuandika. Mwaka 2003 Shirika la Umoja wa Mataifa lilizindua rasmi muongo wa kuzipa msukumo harakati za kuiongeza idadi ya watu wanaoweza kusoma na kuandika ifikapo mwaka 2012. Elimu pia ni moja ya malengo ya milenia ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa.

Watoto wa kike wana uwezekano mkubwa zaidi wa kutopata elimu na wengi wao hulazimika kuacha shule mapema pale wazazi wanaposhindwa kuwalipia karo wana wao wote ili waende shule kila wakati.

Katika mchezo huu, Latifa anakabiliwa na tatizo hilo ijapokuwa amekuwa akipata alama nzuri shuleni. Biashara ya Papa Wali imevurugika - jambo linalomlazimu Latifa kuchangia katika shughuli za kila siku za kuyakimu mahitaji ya familia. Wazazi wake Latifa nao hawajui kusoma na kuandika na wanalazimika kuzitathmini athari za kutomsomesha binti yao. Jee, mchango na ushawishi wa kakake Elinam na rafikiye Zakia utaweza kuwa chachu ya mabadiliko? Ipi hatima ya Epiphane, mfanyakazi wa Papa Wali asiyejua kusoma na kuandika?

Michezo ya Noa Bongo: Jenga Maisha Yako inaweza kusikilizwa katika lugha sita tofauti: Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kihabeshi. Mradi huu unaungwa mkono na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com