1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Msichana Jasiri

Kila msichana ana nafasi sawa kuwa jasiri - Msichana Jasiri!

Kuna mengi ya kujifunza kuhusu kuwa Msichana Jasiri. Vipindi hivi vinakupa fursa ya kusikia ujasiri wa msichana na mchango mkubwa anaoufanya katika jamii. Utasikia jinsi wazazi wanavyoweza kugundua ujasiri wao katika kumlea mtoto wa kike ajitambue kama msichana anayekubalika, anayependwa na mwenye uwezo mkubwa wa kufanikisha ndoto yake ya maisha. Kila msichana ana hatima yake maalumu na ameumbwa na kupewa uwezo kuitimimiza ndoto yake. Msingi muhimu ni mahusiano mema kati ya wazazi na wasichana wao kuwapa makuzi mema. Msichana Jasiri ni muwazi, anaomba msaada anapohitaji, ana upendo na yuko tayari kujitoa kuwahudumia wengine. Ni shujaa!

Onesha makala zaidi