1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshambuliaji wa msikiti New Zealand kufungwa maisha?

Deo Kaji Makomba
24 Agosti 2020

Brenton Tarrant, mzungu anayeamini katika ubaguzi wa rangi aliyewaua waumini 51 wa dini ya Kiislamu huko New Zealand anakabiliwa na kifungo cha maisha jela bila msamaha.

https://p.dw.com/p/3hQyO
Neuseeland Brenton Harrison Tarrant Verurteilung
Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Kirk-Anderson

Mahakama huko New Zealand inatarajia kusikiliza ushahidi kutoka kwa manusura 66 wa tukio hilo, wakati wa siku nne za kusikilizwa hukumu yake. 

Hukumu ya mtu aliyekuwa na bunduki na kumimina risasi na kisha kuwauwa waumini wa dini ya Kiislamu 51 katika shambulio kubwa na baya zaidi huko New Zealand iliendelea Jumatatu chini ya ulinzi mkali.

Mzungu raia wa Australia anayeamini katika ubaguzi wa rangi, Brenton Tarrant, alionyesha hisia kidogo wakati alipoonekana mbele ya mahakama kuu akiwa amefungwa mikono yake na akiwa amevalia nguo za kijivu za magereza.

Tarrant amekiri mashitaka yanayomkabili ya mauaji ya watu 51, mashitaka 40 ya kujaribu na shitaka moja la kutenda kitendo cha kigaidi. Wanasheria nchini humo wanatarajia Tarrant kuwa mtu wa kwanza katika historia ya New Zealand kufungwa jela maisha yote bila msamaha.

Neuseeland Christchurch | Urteilsverkündung gegen Christchurch-Attentäter
Familia na manusura wa shambulizi la msikiti wa Christchurc wakiwa nje ya mahakamaPicha: picture-alliance/AP Photo/M. Baker

Usikilizwaji wa kesi hiyo ulifunguliwa na waendesha mashitaka wakielezea shambulio hilo kwa mukhtasari wa kurasa 26, maafisa katika mahakama hiyo wakielezea kile kilichotokea siku hiyo ya tukio.

Mnamo Machi 15 mwaka 2019, Tarrant mwenye umri wa miaka 29 aliwafyatulia risasi waumini wa dini ya Kiislamu katika misikiti miwili huko Christchurch wakati wa sala ya Ijumaa, na kutangaza tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii. Pia alichapisha mtandaoni malengo yake ya kufanya tukio hilo muda mfupi kabla ya kuwamiminia risasi waumini hao wa Kiislamu.

Mwendesha mashitaka mkuu Barnaby Hawes alisema mshambuliaji huyo alipanga shambulio lake katika msikiti wa Al Noor uliopo katika jiji hilo wakati idadi kubwa ya watu itakapokuwepo. Alirusha angani ndege zisizokuwa na rubani kutokea chini mapema miezi miwili, akizingatia eneo la milango ya kuingia na kutoka.

Siku ya kwanza ya siku nne za kusikilizwa kwa kesi hiyo pia ilikuwa ni fursa ya kwanza kwa marafiki na jamaa wa waathiriwa kumuona uso kwa uso mshambuliaji huyo.

Maysoon Salama, mama mwenye umri wa Atta Elayyan mwenye umri wa miaka 33, aliyeuwawa katika shambulio hilo, alisema, "Umeua ubinadamu wako mwenyewe, na sidhani ulimwengu utakusamehe kwa uhalifu wako wa kutisha, ulidhani unaweza kutuvunja. Umeshindwa vibaya."

Jaji wa mahakama kuu Cameron Mander amepangwa kusikiliza taarifa kutoka kwa waathirika 66 wakati wa kesi hiyo kwa siku nne. Tarrant atafanya uwasilishaji wa hoja za kujitetea mwenyewe kabla uamuzi.

Neuseeland I COVID-19 I Jacinda Ardern
Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Arden asema itakuw ani wiki ngumu kwa taifa hilo.Picha: Getty Images/AFP/M. Melville

Vyombo vya habari vimepigwa marufuku kuripoti moja kwa moja kesi hiyo kutoka katika chumba cha mahakama ili kuhakikisha kwamba uenezi wowote wa kibaguzi wa Tarrant, wakati yuko kizimbani, haupatikani hadharani.

Vizuizi pia viko mahali kwa waandishi wa habari ni kipi wanaweza kuripoti. Ukiukaji wowote wa sheria hizo unaweza kusababisha kudharau mashtaka ya mahakama.

Waziri Mkuu Jacinda Ardern alisema, "Itakuwa ni wiki ngumu kwa wengi. Sidhani kama kuna kitu ninachoweza kusema ambacho kitafanya kutuliza jinsi kipindi hicho kitakavyokuwa," aliwaambia waandishi wa habari.”

Kulikuwa na uwepo mkubwa wa polisi nje ya ukumbi wa mahakama mapema Jumatatu na mbwa wanaofuatilia wakinusa mistari ya wafanyakazi wa mahakama na vyombo vya habari vikiwa kwenye vituo vya usalama.

Wataalam wa afya ya akili pia walikuwa wakisubiri.

Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti kwamba kikosi cha askari hodari wa kulenga shabaha kilikuwa kwenye paa la mahakama hiyo. Kesi hiyo inatafsiriwa moja kwa moja katika lugha nane ili kutosheleza jamii ya Waislamu wa New Zealand.

Soma Zaidi: Mshukiwa wa mauaji ya New Zealand afikishwa mahakamani

DW