Msako mkali waendeshwa mjini Nairobi | Matukio ya Afrika | DW | 10.04.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Msako mkali waendeshwa mjini Nairobi

Serikali ya Kenya imekuwa ikiendesha msako mkali mjini Nairobi baada ya mashambulizi ya kigaidi ili kujaribu kudhibiti hali ya usalama nchini humo.

Kufuatia msako huo, mamia ya washukiwa wamekamatwa na polisi na wengi wanazuiwa katika ukumbi wa Kasarani kwa kukosa vibali vya kuwemo nchini Kenya kihalali miongoni mwa makosa mengine. Mashirika ya kutetea haki za binadamu na viongozi kutoka jamii ya wasomali wameishutumu sana hatua hiyo ya serikali. Hapo jana wizara ya usalama ilitangaza kuwa raia 83 wakisomali ambao hawakuwa na vibali wamerejeshwa Somalia. Caro Robi amezungumza na msemaji wa shirika la kushughulikia maslahi ya wakimbizi UNHCR nchini Kenya Emmanuel Nyabera na kwanza alimuuliza mtazamo wa shirika hilo kuhusu zoezi hilo linaoloendeshwa na Kenya. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikio hapo chini.

Mwandishi:Caro Robi

Mhariri: Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada