1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpizani wa Cameroon asema madikteta hawataki maandamano

Sekione Kitojo
22 Septemba 2020

Maurice Kamto mmoja kati ya wanasiasa  wapinzani  ambao ni msemaji sana, na  kiongozi wa  vuguvugu  la  uamsho nchini  Cameroon amekuwa  akiwahimiza  waungaji wake  mkono kujitokeza kwa ajili  ya maandamano  ya  amani.

https://p.dw.com/p/3iqvH
Frankreich Paris |  kamerunischer Oppositioneller Maurice Kamto
Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon Maurice Kamto Picha: DW/E. Topona

Mkosoaji  huyo  mkubwa  wa  serikali  anadai kuwa  rais  wa  muda  mrefu Paul Biya ajizulu  na  kuruhusu yafayike mageuzi  ya  sheria  za  uchaguzi. Katika  mahojiano  maalum  na  DW, Kamto  anazungumzia juu  ya  maandamano  na  maono  yake kwa  ajili ya  taifa  hilo lenye  matatizo  la  Afrika  ya  kati.

Der kamerunische Oppositionspolitiker Maurice Kamto spricht am 30. Januar 2019 in Paris vor den Medien
Maurice Kamto kiongozi wa upinzani nchini CameroonPicha: DW/M. Mefo

Alipoulizwa  kuhusu  kile  anachotaka  kufanikisha  kupitia  maandamano hayo, Maurice Kamto  alisema , kuna kuna  mambo  mawili makuu. La kwanza  ni  kusitisha  mara  moja  umwagaji  damu katika  eneo  la kaskazini  magharibi  na  kusini  magharibi  kwa  njia  ya  kusitisha mapigano. Unaweza  kufanikisha usitishaji  mapigano  kwa  njia  mbili tofauti.  Ama  majeshi ya  taifa , jeshi  la  Cameroon , linalazimika  kuwa na  mawasiliano  na  kundi  lenye  silaha  na  kukamilisha  usitishaji mapigano. Ama wanaweza  kutangaza  wenyewe  tu kusitisha  mapigano na  kuangalia  iwapo makundi  yenye  silaha  yatatekeleza  makubalinao hayo  ya  kusitisha  mapigano  ama  la.

Nafikiri  ni  njia nzuri kufanya  hivyo  haraka. Iwapo hawataki  kuonekana kuwa  ni  dhaifu, kwasababu  wanajaribu  kujadiliana  na  makundi yenye  silaha, , wanaweza  tu  kusema kwa  wiki  mbili  zinazokuja, tutayarejesha  majeshi  yetu  katika  kambi, na  tutaona jinsi  makundi yenye  silaha yatakavyochukua  uamuzi.

Hii  kwetu  na mimi, ni  njia  bora  kabisa  ya  kufanikisha  usitishaji mapigano  na  kuzuwia  umwagikaji  wa  damu na  vita  vya  kijinga katika  eneo  la  kaskazini  magharibi na  kusini  magharibi mwa Cameroon.

Frankreich Versammlung kamerunische Oppositionelle um Maurice Kamto
Maelfu ya watu wakijumuika katika eneo la Place de la Republique mjini Paris kumsikiliza Maurice KamtoPicha: DW/M.Mefo

Mfumo wa uchaguzi

Nafasi ya  pili ni  mageuzi ya  mfumo  wa  uchaguzi kwasababu tumekuwa  tukitekeleza mfumo  wa  sasa  wa  uchaguzi tangu mwaka 2012 na  tumeweza kupata  matokeo  yale  yale, ikiwa  na  maana kupingwa  kwa  matokeo  ya  uchaguzi. Ndio  sababu  hatukuweza kuingia  katika uchaguzi  wa  Februari  mwaka  2020  kwasababu  njia ile  ile  itatoa  matokeo  yale  yale. Hadi  pale  utakapobadilisha  mfumo wa  uchaguzi, tutakuwa na  matokeo  yale  yale kila  wakati tunapotayarisha  uchaguzi  nchini  Cameroon.

Umewahi kuona  wapi utawala  wa  kidikteta  ukiyaona  maandamano kama ni haki  ya  kisheria? Maurice Kamto  alijibu  hivyo  baada  ya kuulizwa  kwamba  anazungumzia  kuhusu  kuzuwia  umwagaji  damu, na maafisa  nchini  humo  wanasema  maandamano  ni  kinyume na  sheria na  kwamba  majeshi  ya  usalama , "yatachukua  hatua  zote  stahili kuweka  utulivu na  kulinda  sheria."

Maandamano

Haoni kwamba  anawaweka waungaji  wake  mkono  katika  hatari? Kamto  alisema  ni sheria  gani ambayo inakiukwa  kwa  kufanya  maandamano ? Katiba  ya  Cameroon iko  wazi  kabisa  kuhusu  hilo. Uhuru  wa  kukusanyika, kuhutubia, na maandamano  kwa  mujibu  wa   sheria.

Kamerun Haftentlassung - Maurice Kamto
Malefu ya watu wakimsalimia kiongozi wa upunzani nchini Cameroon Maurice Kamto mjini YaoundePicha: AFP

Ina  maana  kwamba unatekeleza  kwa  mujibu wa  sheria, na  sio  kwamba  sheria  ama maafisa  wa  utawala  wanaweza  kupiga  marufuku uhuru  uliomo  katika katiba. Mwishoni  mwa  hayo, katiba  hiyo  hiyo  inasema  kwamba serikali  itahakikisha  kila  mtu  anatumia  sheria  hizi  zinazomhusu  kila raia. Kwa  hiyo  hakuna  ukiukaji wa  sheria  yoyote  hapo.

Unapozungumzia watu kuwaweka  katika  hatari , ni ujumbe  wa  jeshi ama  serikali  kufyatulia watu risasi ambao  wanataka  kuandamana kwa amani ? Tunafikiri  kwamba  njia  pekee kwetu kueleza  kutokubaliana , hasira zetu, mfadhaiko wetu kwa serikali  hii ni  kuandamana kwa amani. Kwa  kuwa  hatuwezi  kufanya  kupitia  uchaguzi  ulio huru  na wa  haki, hatutaweza  kwenda  barabarani  kucheza. Tunakwenda  huko kwasababu  tuko  na  furaha  kwenda  huko. Tungependa  kusisisitiza hilo.