Mourinho: Torres bado ataichezea Chelsea
4 Aprili 2014Matangazo
Mourinho alimchagua Andre Schuerrle badala ya Mhispania huyo wakati walipofungwa magoli matatu kwa moja na kisha baadaye akakiri kuwa hakufurahishwa na mchezo wa karibu wa washambuliaji wake.
Mreno huyo hajaficha lolote kuhusu nia ya Chelsea kumnunua mshambuliaji wa tajriba ya juu wakati wa kipindi kijacho cha uhamisho, na kuzusha maswali kuhusu mustakabali wa Torres.
Mourinho amesema Torres ameonyesha mchango wake tangu alipojiunga na Chelsea, lakini anaweza kuongea bidii ili kuendelea kufunga magoli. Chelsea wanacheza baadaye leo dhidi ya Stoke City wakilenga kuyafufua matumaini yao ya kutwaa taji la Premier League
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman