Mourinho: nina uhusiano mzuri na wenzangu | Michezo | DW | 14.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mourinho: nina uhusiano mzuri na wenzangu

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Kandanda ya England Chelsea wanasafiri na Manchester City, makamu bingwa wa msimu uliopita, huku kocha Jose Mourinho akigubikwa na mgogoro unaomhusu daktari wa timu Eva Carneiro

Carneiro mwenye umri wa miaka 41alizomewa na Mourinho baada ya kukimbia kuingia uwanjani kumtibu Hazard baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Swansea.

Hali hiyo iliifanya Chelsea kubaki na wachezaji nane uwanjani baada ya mlinda mlango Thibaut Courtois kuzawadiwa kadi nyekundu. Jose amethibitisha kuwa carneiro hatohudhuria mechi ya kesho

Mourinho hata hivyo hajafichua ni kwa nini alichukua uamuzi huo lakini amesisitiza kuwa ana uhusiano mzuri sana na kitengo cha madaktari wa Chelsea. Katika mchuano mwingine wa kesho, mlinda mlango Petr Cech atatumai kuwa na mchuano wa pili mzuri katika klabu yake ya Arsenal, kuliko wa kwanza ambapo alilaumiwa kwa magoli yote mawili, wakati Arsenal itakapokutana na Crystal Palace. Arsenal iliduwazwa na West Ham kwa kufungwa magoli mawili bila jibu wikendi iliyopita na Wenger anasema muhimu ni namna vijana wake watakavyojinyanyua kutokana na kichapo hicho

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Daniel Gakuba