1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Monaco yakamilisha usajili wa Kevin Volland

Sylvia Mwehozi
2 Septemba 2020

Klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa imemsajili mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani Kevin Volland kutoka Bayer Leverkusen kwa mkataba wa miaka minne hadi mwaka 2024.

https://p.dw.com/p/3htvJ
Deutschland Bundesliga Bayer Leverkusen v Mainz 05
Picha: Getty Images/AFP/M. Meissner

Klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa imemsajili mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani Kevin Volland kutoka Bayer Leverkusen kwa mkataba wa miaka minne hadi mwaka 2024. "Nimefurahi kujiunga na klabu hii yenye historia kubwa na yenye kiu ya mafanikio", alisema Volland.

"Nimekuwa nikifuatilia matokeo ya awali ya timu hii na hivi sasa ninafurahi kujiunga na klabu hii na kufanya kazi nayo katika kuleta ujuzi wangu kwenye timu", aliongeza Volland.

Monaco iliyokuwa ikinolewa na kocha wa zamani wa Bayern Munich Niko Kovac inasemekana kuwa imetoa kibunda cha euro milioni 20 kwa ajili ya kumpata mshambuliaji huyo. Volland alijiunga na Levekusen mwaka 2016 akitokea Hoffenheim na amefumania nyavu mara 77 katika michezo 247 ya Bundesliga.