Mohammed Abdul-Rahman | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 20.04.2017
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu ya DW Kiswahili

Mohammed Abdul-Rahman

Mfahamu Mohammed Abdul-Rahman, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW

 1. Nchi ninayotokea: Tanzania
 2. Mwaka nilipojiunga na DW: 1980
 3. Nilivyojiunga na DW: Nilituma maombi na nikakubaliwa mkataba wa miaka miwili na hatimae kurefushiwa mara mbili kabla ya kupata mkataba wa kudumu.
 4. Kwanini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Ni kitu kilichonivutia tangu utotoni  na kuvutiwa  na watangazaji mashuhuri wa  enzi hizo  wa redio za kimataifa. Baadae nikajifunza  fani hiyo.
 5. Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Kuzijua alau kwa  kiwango fulani siasa za dunia, kufuatilia matukio duniani, uadilifu na kutoelemea upande wowote katika ukusanyaji na utoaji habari.
 6. Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: Kutokana na uzoefu wa miaka mingi hakuna changamoto kubwa isipokuwa tu pale unapokuwa ukiripoti juu ya ripoti inayogonga vichwa vya habari wakati huo, huku ukijitahidi kuhakikisha inawafikia haraka wasikilizaji.
 7. Tukio la kihistoria ambalo sitalisahau:  Kuanguka kwa ukuta wa Berlin. Pili: Nilipokutana na Rais Yoweri Museveni na waziri wake Paul Semogerege mjini Bonn miezi michache baada ya Museveni kutwaa madaraka 1986. Tatu: Mazungumzo yangu na Rais Laurent Desire Kabila ofisini kwake miini Kinshasa na mwezi mmoja na nusu baadae akauwawa.
 8. Mtu ambaye ningependa kumhoji: Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com