1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlinda amani wa UN auawa Kongo

6 Februari 2023

Mwanajeshi mmoja wa Afrika Kusini anayehudumu kwenye Kikosi cha Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, ameuawa.

https://p.dw.com/p/4N8uB
Demokratische Republik Kongo | MONUSCO Blauhelm
Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Na mwenzaake kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya helikopta yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemorasi ya Kongo hapo jana.

Msemaji wa MONUSCO, Amadou Ba, amesema ndege hiyo ilishambuliwa majira ya saa tisa alasiri, wakati ikiwa safarini kwenda mjini Goma, ambako iliweza kutua.

Jeshi la Afrika Kusini pia limethibitisha tukio hilo, likisema limo katika mchakato wa kutoa taarifa kwa familia za wanajeshi waliohusika katika mkasa huo.

Mkuu wa MONUSCO amelaani shambulio dhidi ya ndege hiyo iliyokuwa na nembo ya Umoja wa Mataifa, huku Katibu Mkuu wa Umoja huo, AntonioGuterres, akizitaka mamlaka nchini Kongo kuchunguza shambulio hilo na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria.