Mke wa Mursi ajitokeza hadharani | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.08.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mke wa Mursi ajitokeza hadharani

Mke wa rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohammed Mursi amewaambia maelfu ya wafuasi wa rais huyo kuwa waendelee na upinzani dhidi ya kitisho cha kwa viongozi wa serikali ya mpito kwamba watawaondoa kwa nguvu.

epa03816743 Egyptians supporting ousted president Morsi (depicted in poster) perform Eid al-Fitr prayer at their continuing sit-in location, near Rabaa Adawiya mosque, Cairo, Egypt, 08 August 2013. Muslims worldwide celebrate the Eid al-Fitr holidays which mark the end of the Muslims' Holy fasting month of Ramadan. Eid al-Fitr 2013 celebrations start on 08 August and last for most countries from two to four days during which children get new clothes, often their first pocket money and visit family members with their parents exchanging greetings and some of the many pastries prepared for the occasion. EPA/AHMED RADAMAN

Waungaji mkono wa Mursi mjini Cairo

Naglaa Mahmoud mke wa rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Mursi amewaambia maelfu ya waungaji mkono mume wake jana(08.08.2013) waendelee na upinzani wao bila kujadi kitisho hicho kilichotolewa na viongozi wa serikali inayoungwa mkono na jeshi.

Naglaa Mahmoud alijitokeza kwa mara ya kwanza tangu jeshi kufanya mapinduzi hapo Julai 3, ambayo yalifuatia maandamano ya umma , wakitaka mume wake aondolewe kutoka madarakani.

An Egyptian girl chants slogans as she joins supporters of Egypt's ousted President Mohammed Morsi as they celebrate the first day of the Eid al-Fitr holiday, marking the end of the Muslim holy fasting month of Ramadan outside Rabaah al-Adawiya mosque, where protesters have installed a camp and hold daily rallies in Nasr City, Cairo, Egypt, Wednesday, Aug. 8, 2013. This year's holiday of Eid al-Fitr was overshadowed by the deep divisions in Egypt, with the interim government planning to celebrate the festival with outdoor prayers in town center squares and Morsi's supporters marking the holiday with their own protest gatherings, including the two major sit-in by the Islamists in Cairo. (AP Photo/Khalil Hamra)

waungaji mkono Mohammed Mursi katika maandamano mjini Cairo 8.8.2013

Hapo kabla vyombo vya habari vya Misri vilieleza kuwa Naglaa alikuwa akishikiliwa pamoja na mume wake katika eneo ambalo halijulikani pamoja na watoto wake.

Apandishwa jukwaani

Waandamanaji katika eneo la Nasir mjini Cairo walishangiria alipowasili na kupanda jukwaani. Hakusema alikuwa wapi tangu yalipofanyika mapinduzi. Waandamanaji walisherehekea sikukuu ya Idd el fitr katika eneo hilo la Nasr, na mmoja kati ya waandamanaji alisema.

"Nimekuja hapa na kushiriki Idd pamoja na kundi hili ambalo limekuwa likikandamizwa, lakini nilitaka kuwapo kwangu hapa kuwe ni ujumbe kuwa tuko pamoja dhidi ya wale waliofanya mapinduzi."

Photo title: soldiers and feast Photo discription: soldiers and civilians in the feast morning near tahrir sq. Photo date: 8, 8, 2013 Photo place: cairo. Egypt Photo: nael eltoukhy, DW-Korrespondent

Sherehe za Eid Al-fitr mjini Cairo

Musri anashikiliwa pamoja na wasaidizi wake wa ngazi ya juu, idadi kubwa wakiwa wamehamishiwa katika jela hivi karibuni kusini mwa mji wa Cairo.

Wanakabiliwa na mashitaka ikiwa ni pamoja na kuchochea ghasia katika matukio mbali mbali ambayo yamesababisha ghasia kubwa zilizomwaga damu mitaani katika muda wa mwaka mmoja wa utawala wa Mursi.

Watoto wa Mursi

Watoto wa Mursi pia wamejiunga na maandamano hayo ya kundi la Udugu wa Kiislamu na wametoa wito wa kuachiliwa baba yao.

An image grab taken from Egyptian state television Al-Masriya on July 1, 2013 shows an image of Egypt's Defence Minister and armed forces chief General Abdul Fatah Al-Sissi as a statement was read warning that Egypt's armed forces will intervene if the people's demands are not met within 48 hours, after millions took to the streets to demand the resignation of Islamist President Mohamed Morsi. AFP PHOTO / AL-MASRIYA TV == EDITOR'S NOTE - RESTRICTED TO EDITORIAL USE - MANDATORY CREDIT AFP PHOTO / AL-MASRIYA TV - NO MARKETING NO ADVERTISING CAMPAIGNS - DISTRIBUTED AS A SERVICE TO CLIENTS == (Photo credit should read -/AFP/Getty Images)

Mkuu wa jeshi la Misri Abdel Fattah al-Sissi

Viongozi wa mpito wa Misri pamoja na jeshi wamesema kuwa wataendelea na mpango wao wa haraka wa mpito ambao unatoa fursa ya uchaguzi ifikapo mapema mwaka ujao.Nae kkiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameonya leo kwamba mzozo wa kisiasa nchini Misri unaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Khamenei amesema kuwa matukio nchini Misri yanatia wasi wasi.

Wanadiplomasia kutoka mataifa ya kigeni pamoja na wizara za mambo ya kigeni za mataifa ya kiarabu wamejaribu kupatanisha na kufikia suluhisho la amani kati ya pande hizo mbili.

U.S. Senators John McCain, left, and Lindsey Graham, R-S.C., right, hold a press conference in Cairo, Egypt, Tuesday, Aug. 6, 2013. The two senior U.S. senators have urged Egypt's military-backed government to release detained members of the Muslim Brotherhood before starting negotiations. Tuesday's comments came after McCain and Graham met with top military and civilian leaders in Cairo as part of a flurry of international efforts to resolve a standoff with supporters of the ousted president Mohammed Morsi. (AP Photo/Amr Nabil)

Mkutano na waandishi habari seneta wa Marekani John McCain(shoto) na Lindsey Graham(kulia)

Hata hivyo ziara ya hivi karibuni ya seneta wa Marekani John McCain na Lindsey Graham ilizusha hasira wakati maseneta hao walipotoa wito wa kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa , wakiwa na maana viongozi wa udugu wa Kiislamu ambao wanatuhumiwa kwa kuchochea ghasia.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape

Mhariri : Abdul-Rahman, Mohammed

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com