1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubora wa zao la Kakao kuzingatiwa.

20 Aprili 2018

Wazalishaji wa chokoleti duniani wanasema wanahitaji kununua Kakao katika mpango wa soko huru n alenye maadili, wakati wanafanya mianya ya usambazaji wa zao hilo kuwa ya kimaadili ifikapo mwaka 2020.

https://p.dw.com/p/2wQ84
Elfenbeinküste Kakao Anbau Ernte
Picha: Reuters/L. Gnago

Makampuni makubwa ya kutengeneza chokoleti duniani yametakiwa kuwasaidia wakulima kuwa na mipango ya kimaadii ya uzalishaji wa zao hilo ili waweze kupata mapato yanayoendana na uzalishaji. Licha ya jitihada za muda mrefu za kuwa na soko huru na lenye maadili la zao la kakao, lakini bado wakulima hao wameshindwa kufikia malengo yanayotakiwa.

Wazalishaji wa chokoleti duniani, wananunua kakao zaidi katika miradi iliyopangwa ya kuondokana na umaskini wakati wanafanya mianya yao ya usambazaji wa bidhaa hiyo kuwa ya kimaadili ifikapo mwaka 2020. 

Tatizo lililopo kwa wakulima wa zao la kakao linalotumika kutengeza bidhaa ya chokoleti ni malipo wanayoyapata kutokana na maharage yanayouzwa chini ya mojawapo ya mipango endelevu ya kimaadili. Juhudi za kuzuia ukataji miti, ajira kwa watoto na mishahara midogo katika viwanda vya kakao bado hazijatosha kuzuia kuendelea kwa matukio hayo. 
Mipango ya kulifanya zao la kakao kuwa bora ifikapo 2020 yaendelea. 

Kakao iliyowekwa kwenye vifungashio tayari kwa mauzo.
Kakao iliyowekwa kwenye vifungashio tayari kwa mauzo.Picha: Reuters/L. Gnago

Wazalishaji wakubwa wa Kakao wameahidi kununua zao hilo kama litakuwa limethibishwa  kuwa na ubora endelevu ifikapo mwaka 2020. Kiasi cha kakao kuuzwa kupitia mipango kama vile biashara huru na haki, imeongezeka kwa kasi katika miaka michache iliyopita wakati makampuni yakifanya kazi kufikia malengo yao.

Mauzo ya kakao kutoka kiwango cha tatu cha kuthibitishwa ni kuanzia tani laki tano sitini na nne elfu mia saba sitini na tisa kwa mwaka 2013 kwenda mpaka tani laki tisa hamsini na tatu elfu mia nne hamsini na nane kwa mwaka 2016, hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 20 ya ugavi wa kimataifa.

Malipo ya kakao yenye ubora  ambayo wakulima wanapokea kutoka kwa wanunuzi imeshuka kutoka dola 150 kwa mwaka 2013 dola 111 kwa mwaka 2017, na hiyo ni kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa wiki hii. 

Miongoni mwa sababu zilizochangia malipo ya kakao kushuka ni usambazaji ulliopitiliza ambayo imesukuma bei za dunia kushuka kwa miaka tisa mfululizo hadi kufikia mwaka jana 2017.

Lakini mipango ya kimadili inayoandaliwa inaweza kuwasaidia wakulima kuepuka umaskini kupitia mauzo ya zao la kakao na kuhakikisha kuwa fedha nyingi zinawafikia wakullima moja kwa moja.

Wakosoaji wanasema mafanikio yake yamekuwa sehemu ya kuangusha thamani ya zao hilo kwa sababu haifai makampuni kuwalipa wakulima kiasi cha bei fulani kwa zao hilo.

Mkulima wa Kakao akilalamiki amkataba mbovu wa mauzo.
Mkulima wa Kakao akilalamikia mkataba mbovu wa mauzo.Picha: A. Duval Smith

Wakulima wa zao hilo wanalalamikia bei.

Kwa upande mwingine biashara huru inasisitiza juu ya kuweka vigezo vya bei vitakavyokuwa na manufaa kwa wakulima na wanunuzi. Mtazamo wa wanunuzi ni kwamba malipo huwa ni kidogo kwa bidhaa ile ile ambayo ingeweza kununuliwa kwa malipo ya juu zaidi. Vikundi vya kujitegemea yenye vyeti huwa yanatoa kibali kwa wakulima ambao kakao yao imelimwa katika viwango vyenye ubora.

Lakini biashara huru bado inapiganiwa ili kupanua wigo wake, lakini mfano hauonekani katika makampuni makubwa ya chakleti kipindi hiki inapotazamiwa kuyafikia malengo ya uuzaji wa kakao bora ifikapo mwaka 2020.

"'Mwaka 2020 haupo mbali wote wanatakiwa kuongeza manunuzi yao ya kakao yenye ubora," alisema mmoja wa wanunuzi wa kakao.

Mwaka 2016 wakulima waliuza asilimia 54 katika tani milioni moja nuktambili za kakao iliyobora katika kampuni ya kununua kakao ya UTZ kupitia mpango wa mauzo bora na kufikia asilimia 80 ya mauzo kwa mwaka 2017 kama ambavyo takwimu za mauzo zinavyoonesha.

Wakati sehemu ya soko huru la biashara inakuwa haijawahi kabisa kupunguza gharama, na haina mipango ya kufanya hivyo katika mapitio yake ya mwaka huu licha ya kuwa ni muhimu kwa kuboresha ustawi na kujenga mifano ya biashara endelevu.

Mwandishi: Veronica Natalis/ Reuters
Mhariri: Josephat Charo