Kila nafsi itaonja mauti. Hiyo ndio ada ya mwisho kwa binadamu yeyote. Lakini hata ukweli huu unapokuwa wazi, namna miili inavyostiriwa na sherehe zinazoambatana na mazishi hayo ni tofauti katika jamii mbali mbali, huku nyingi ya mila na sherehe hizo zikiwa tatanishi. Makala ya utamaduni na sanaa inazitazama mila na taratibu za jamii mbali mbali kuhusiana na mazishi. Ungana na Tatu Karema.