1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Migogoro na majanga vimeacha watu milioni 76 bila makazi

14 Mei 2024

Migogoro na majanga ya asili yamesababisha takriban watu milioni 76 kuachwa bila makaazi ndani ya nchi zao katika kipindi cha mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4fqdg
Mafuriko huko Canoas, Rio Grande do Sul, Brazili
Muonekano wa picha ya juu unaoonyesha kitongoji cha Harmonia kilichofurika katika jiji la Canoas, jimbo la Rio Grande do Sul, Brazili, Mei 13, 2024.Picha: Nelson Almeida/AFP

Vita katika nchi za Sudan Kongo na Mashariki ya Kati vimesababisha thuluthi mbili ya watu kuhama kwa mujibu wa shirika kubwa  linalofuatilia masuala ya uhamiaji duniani. Ripoti ya shirika hilo imebaini kwamba idadi ya wakimbizi wa ndani imefikia asilimia 50 katika kipindi cha miaka 5 iliyopita na imeongezeka mara mbili katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Ripoti hiyo imechapishwa kutokana na  utafiti uliofuatilia nyendo za watu milioni 46.9 katika mwaka 2023 baada yamatukio ya majanga ya asili kama mafuriko.Kiasi ya watu milioni 75.9 wanaishi katika mazingira ya kuwa wakimbizi wa ndani katika mataifa yao kufikia mwishoni mwa mwaka jana na wengi wako katika mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara,barani Afrika.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW