Michwzo mwishoni mwa wiki | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 21.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Michwzo mwishoni mwa wiki

Jumamosi hii ni finali ya kombe la afrika mashariki na kati baina ya mabingwa Sudan na Ruanda mjini Dar-es-salaam.

Jumamosi hii ni finali ya kombe la challenge Cup-kombe la Cecafa-shirikisho la dimba la Afrika mashariki na kati baina ya mabingwa watetezu Sudan na Ruanda ilioipiga kumbo nje ya finali Uganda.

Hamburg na Nuremberg, zinajiunga na Bayern Munich viongozi wa Bundesliga-Ligi ya Ujerumani na Bayer Leverkusen katika duru ijayo ya kombe la UEFA-kombe la shirikisho la dimba la Ulaya.Arsenal, inarudi uwanjani jumamosi jioni ikisaka pointi 3 kutoka Tottenham Hotspurs kabla Manchester United kuingia jumapili uwanjani na Everton wakati Chelsea ina miadi na Blackburn.

Bundesliga-ligi ya Ujerumani imekwenda likizo ya X-masi na mwaka mpya hadi Februari mosi pale viongozi wa Ligi Bayern munich watakapofunga safari hadi mashariki kupambana na Hansa Rostock.

Kesho jumamosi, asie na mwana kweli aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano –uwanja wa taifa Dar-es-salaam –kituo cha finali ya Kombe la Challenge kati ya mabingwa watetezi-Sudan na Ruanda.

Kombe litaelekea wapi ?

Wengi walitazamia finali ya leo ingelikuwa kati ya Waganda na Wasudani,lakini mpira unadunda na baada ya maajabu ya Zanzibar heroes iliomudu sare na Sudan,ikaitoa Ethiopia na kutoa changamoto kali kwa Ruanda hadi mikwaju ya penalty ilipoamua hatima yao majuzi,Ruanda imewatoa pia waganda.

Ilikua bao lao wenyewe waganda juzi na nahodha wao wenyewe Andrew Mwesigwa lililoizamisha jahazi ya Ugandan Cranes. Ruanda imetwaa kombe hili mara moja tu 1999 na leo Kagame Cup ni lao ?

Katkka Ligi ya Uingereza mapamban o mengine hii leo ni kati ya Aston villa na Manchester City ,Bolton Wanderers wanaumana na Birmingham City ,Fulham na Wigan Athletics wakati Liverpool inakaribisha nyumbani pottsmouth.Kesho Newcastle united inachuana na Derby County.

Katika La Liga-Ligi ya spain –Real zaragoza wanacheza leo na Valencia wakati Almeria wanaonana na Getafe huku Sevilla wakiwa nyumbani na wageni wao Santander.Macho yote lakini yatakodolewa kesho jumapili pale mahasimu wakubwa 2 wa nyumbani Real Madrid watakapokumbana na FC Barcelona.

Katika Ligi ya Itali-Serie A, Genoa inaonana leo na Parma huku AS Roma wakiw nyumbani kuwakaribisha Sampdoria.Macho lakini huko Itali, yanakodolewa mpambano wa kufa-kupona kati ya mahasimu 2 wa mtaani-mabingwa wa dunia na Ulaya AC Milan na Inter Milan. Nisingethubutu kuagua matokeo yake.

Katika ringi ya mabondia, imetangazwa kwamba changamoto ya kuania taji la wezani wa juu ulimwenguni la WBC kati ya bingwa mrusi Oleg Maskaev na Mnigeria Samuel Peter itakua Machi 8 huko Cancun,Mexico.

Maskaev alikua atete taji lake hilo dhidi ya Peter, oktoba mwaka huu huko Madison Square Gardens, NY lakini alilivunja kutokana na kuumia.

 • Tarehe 21.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CerA
 • Tarehe 21.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CerA
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com