1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wakwamisha maelfu ya abiria Ujerumani

Daniel Gakuba
17 Februari 2023

Wafanyakazi katika viwanja vinane vya ndege nchini Ujerumani wanafanya mgomo leo, wakishinikiza kuongezewa mishahara na kuboreshewa mazingira ya kazi.

https://p.dw.com/p/4Ndtx
Deutschland | Flughafen Frankfurt | Landung Lufthansa Boeing 747-8
Picha: Arne Dedert/dpa/picture alliance

Mgomo huo wa siku nzima ya leo ulioitishwa na chama cha wafanyakazi cha Verdi umeilazimisha kampuni kubwa ya ndege nchini Ujerumani, Lufthansa kufuta safari zipatazo 1300 katika viwanja vya Frankfurt na Munich ambavyo ndivyo vyenye shughuli nyingi zaidi. Viwanja vingine vilivyoathirika vipo katika miji ya Bremen, Dortmund, Hamburg, Hanover, Leipzig na Stuttgart. Makumi kwa maelfu ya wasafiri wanakabiliwa na uwezekano wa safari zao kucheleweshwa au kufutwa kabisa. Shirika la viwanja vya ndege Ujerumani, ADV, limeulaani mgomo likisema haukubaliki, likongeza kuwa utawaathiri wasafiri 295,000 na jumla ya safari za ndege 2,300. Chama cha wafanyakazi cha Verdi kinataka wafanyakazi waongezewe malipo wakati huu ambapo mfumuko wa bei umeshusha thamani ya mishahara yao na kuzidisha ugumu wa maisha.