Mgogoro kuhusu umilikaji wa visiwa baina ya China na Japan | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.09.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mgogoro kuhusu umilikaji wa visiwa baina ya China na Japan

Kwa siku sasa maelfu ya Wachina wamekuwa wakifanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi yao kupinga hatua za Japan kutaka kuvimiliki visiwa vidogo vya Senkaku vilioko katika bahari baina ya nchi hizo mbili.

Waandamanaji wa Kichina wachoma moto bendera ya Japan

Waandamanaji wa Kichina wachoma moto bendera ya Japan

Maandamano hayo, mingine ya hamasa kubwa na yakipita mbele ya ubalozi wa Japan mjini Beijing, yamezusha wasiwasi wa kimataifa na hofu baina ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani. Kuna ripoti kwamba makampuni ya kijapani hivi sasa yanafungwa au kupunguza shughuli zao huko China.

Othman Miraji alizungumza na mwandishi wetu wa Beijing, Fadhili Mpunji, na akamuuliza uhasama huu unaangaliwa kwa kiasi gani huko China.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mahojiano: Othman Miraji/ Fadhili Mpunji

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com