Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Usalama wa bahari unatajwa kuwa mashakani kutokana na shughuli za kibinadamu zinazohatarisha uhai wa viumbe baharini kuendelea kushuhudiwa katika mataifa mengi ulimwenguni hatua inayowatoa hadharani wataalamu wa mazingira na kutoa wito wa harakla kunusu uhai chini ya maji. Vidio na Hawa Bihoga #kurunzi
Mti wa Mgandi ambao ni sehemu ya matambiko katika jamii za kibantu, unaotumiwa pia kama dawa za kiasilia, uko katika hatari ya kukatwa. Wakaazi wa Ngoloka katika kaunti ya Kilifi nchini Kenya wanasema huenda hatua hiyo ikaharibu historia kubwa ya jamii hiyo. #Kurunzi19.01.2020
Tatizo la uhaba wa nafasi za ajira kwa vijana linapoendelea kukumba nchi nyingi, swali linalowatatiza wengi ni njia gani bora kukuza elimu ya ufundi ili kutatua matatizo ya jamii. Lakini pia swali ni ikiwa vijana wanapenda kozi za ufundi au la. Kwenye video hii Veronica Natalis anaangazia umuhimu wa ufundi kushughulikia mahitaji ya jamii.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amedai ushindi katika uchaguzi wa rais, na kutupilia mbali matokeo ya awali yanayomuonyesha rais Yoweri Museveni akiongoza kwa tofauti kubwa.
Hali ya usalama imeimarishwa katika majengo ya bunge mjini Washington, Marekani baada ya kitisho cha maandamano yaliyopangwa kufanywa na wafuasi wa Rais Donald Trump wikendi hii.
Kiongozi mkongwe nchini humo Rais Yoweri Museveni anawania muhula wa sita uongozini japo anakabiliana na upinzani kutoka kwa aliyekuwa nyota wa muziki Robert Kyangulanyi almaarufu Bobi Wine.
Wakati Uganda ikijiandaa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu siku ya Alhamisi, mengi tayari yamejitokeza wakati wa kampeni. Video hii inakukumbusha machache miongoni mwa hayo mengi.
Kuwepo kwa harakati nyingi za kupigania na kutetea haki za wanawake na wasichana kumeongeza au kumepunguza chochote kwenye jamii? Kweli wanawake na wasichana wanatambua haki zao na kusaidika?
Tizama hapa wakaazi takribani 200 wa kisiwa cha Msangamkuu huko Mtwara Tanzania, wanaojitolea kupanda miti ya Mikoko kandokando ya bahari ili kukinusuru kijiji chao kumezwa na maji ya bahari.
Taasisi ya TAI nchini tanzania inayoundwa na vijana wenye vipaji inatumia michoro ya vikaragosi ya chapa tatu ama kwa kimombo 3D animations kuelimisha, kuonya na hata katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia pamoja na usawa kwa watoto wa kike.
Mwekezaji na mwanaharakati wa mazingira kutoka Cape Verde Carlos Silva anataka kusaidia katika utunzaji wa mazingira kwa kutengeneza bidhaa za mapambo zisizokuwa na kemikali wala vihifadhi visivyo vya asilia
Kilimo 'kichuguu' ni aina ya kilimo kinachowafaa wale ambao hawana mashamba makubwa. Katika eneo lako dogo, unajitengenezea kijishamba na kupanda mboga kama ambavyo Veronica Anavyosimulia.
Hatua ya mamia ya wafuasi wa rais wa Marekani Donald Trump kuyavamia majengo ya Bunge la Marekani, maarufu kama Capitol Hill mjini Washington, imesababisha maoni mengi kutolewa kote duniani. #Kurunzi 07/01/2021
Ni afueni kubwa kwa wakaazi wa Likoni mjini Mombasa baada ya daraja hili la kuning’inia kuanza kutumika katika eneo hili la Liwatoni. #Kurunzi 07/01/2021
Wapiga kura nchini Uganda wamo katika pilikapilika za kuhakikisha kuwa majina yao yamo kwenye daftari la shughuli hiyo itakayofanyika Alhamisi tarehe 14 mwezi huu wa Januari 2021.#Kurunzi 07/01/2021
Baada ya shule kufungwa kwa miezi 10 iliyopita nchini Kenya kufuatia janga la virusi vya corona, hatimaye wanafunzi wote sasa wameruhusiwa kurudi shuleni ili kuendelea na masomo yao. Hata hivyo shule zimefunguliwa chini ya masharti mapya kwa lengo la kuzuia maambukizi zaidi kutokea. Thelma Mwadzaya anaeleza zaidi kutoka Nairobi.
Utunzaji wa msitu huu wenye uoto wa asili wa Kiwengwa Pongwe, kaskazini mwa kisiwa cha Unguja, unaweza kuwa juhudi njema yenye dhamira ya kuinusuru jamii. Hapa hupatikana idadi kubwa ya mitishamba ambayo imekuwa ikitumika miaka mingi kwa tiba za asili na ambayo kwa sasa imekuwa haba #Kurunzi
Mahakama jijini London imeamuwa kwamba Julian Assange hawezi kusafirishwa kupelekwa Marekani, uamuzi unaoashiria kwamba kitisho cha mwanzilishi huyo wa mtandao wa WikiLeaks kutumikia kifungo cha miaka 175 kimeondoka, angalau kwa sasa. Kurunzi 04.01.2021.
Rais wa Marekani anayemaliza muda wake, Donald Trump, amenaswa kwenye mazungumzo ya simu akimshinikiza mkuu wa tume ya uchaguzi wa jimbo la Georgia akimtaka amtafutie kura takribani 12,000 zinazohitajika kumpa ushindi kwenye jimbo hilo. #Kurunzi
Umoja wa Mataifa unauorodhesha mkoa wa Shinyanga uliopo kaskazini mwa Tanzania kuwa ni kati ya mikoa inayorekodi idadi ya juu zaidi ya wasichana wanaopata mimba na kuolewa katika umri mdogo. Katika vidio iliyoandaliwa na Veronica Natalis kuna taarifa ya hali ilivyo