1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mechi za kuwania fainali za Kombe la Afrika

Daniel Gakuba
10 Septemba 2018

Mwishoni mwa Juma kumeendelea mechi za kuwania nafasi katika fainali za kombe la Mataifa ya Afrika. Jumla ya michezo nane ilishuhudiwa katika viwanja mbalimbali.

https://p.dw.com/p/34cGI
Angola Stadion des 11. November in Luanda
Picha: Imago/Gallo Images

Jumla ya mechi nane za kuwania nafasi katika fainali za Kombe la Afrika la Mataifa zimechezwa mwishoni mwa Juma. Madagascar ilitoka sare ya magoli 2-2 na Senegal mjini Antananarivo, Sudan Kusini ikatandikwa magoli 3-0 na Mali kwenye uwanja wake wa nyumbani, Ethiopia ikaiangusha Sierra Leoni kwa goli 1-0 mjini Addis Ababa, nayo Kongo Brazzaville ikatoka nguvu sawa na Zimbabwe kwa kufungana bao 1-1. Katika mechi nyingine, Rwanda ililazwa na Ivory Coast magoli 2-1 mjini Kigali, Angola ikatumia vyema uwanja wa nyumbani kuifunga Botswana goli 1-0, Mjini Manzini, Swaziland ambayo sasa inajulikana kama eSwatini ikalambwa magoli 2-0 na Tunisia, na mjini Maseru, Lesotho ilitoka sare ya 1-1 na Cape Verde.