Mchezaji bora wa Bundesliga 2016 | Michezo | DW | 23.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Mchezaji bora wa Bundesliga 2016

Ni mchezaji yupi wa Bundesliga aliyeukonga moyo wako 2016? Ni mmoja kati ya washambuliaji matata au mabeki mahiri? Tunamtafuta mchezaji bora wa mwaka katika Bundesliga na unapaswa kuamua nani atakayeshiriki shidano hili!

Ni rahisi kushiriki. Bonyeza jina la mchezaji umpendaye, andika jina lako, anuani ya posta na nambari yako ya simu – na tayari utakuwa umeshiriki shindano. Kila anayeshiriki ana fursa ya kushinda zawadi nono. Hatimaye tutamtafuta mshindi kati ya washiriki wote atakayepata jezi ya timu anayoipenda katika Bundesliga kutoka kwetu. Fanya hima, tumia kompyuta, tablet au simu yako ya Smartphone na upige kura yako sasa!

Chagua kati ya wachezaji hawa 11

Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund)
Anthony Modeste (1. FC Köln)
Robert Lewandowski (FC Bayern München)
Vedad Ibisevic (Hertha BSC)
Joshua Kimmich (FC Bayern München)
Emil Forsberg (RB Leipzig)
Jerome Boateng (FC Bayern München)
Julian Weigl (Borussia Dortmund)
Javier "Chicharito" Hernandez (Bayer 04 Leverkusen)
Ralf Fährmann (FC Schalke 04)
Sandro Wagner (SV Darmstadt / 1899 Hoffenheim)

Shindano litakamilika 20.01.2017 saa nne na nusu usiku wakati mechi ya duru ya pili ya ligi ya Bundesliga itakapoanza. Uamuzi wetu ni wa mwisho na hakuna haki ya kwenda mahakamani. Tafadhali zingatia masharti yetu ya matumizi.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com