Mbona iwe tu ni Mario Balotelli? | Michezo | DW | 19.12.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Mbona iwe tu ni Mario Balotelli?

Mbona ni mimi tu? Ni kama anakokwenda anaandamwa tu na kashfa, au ni yeye anayeziandamaan kashfa? Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli haonekani kuepuka vichwa vya habari

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Mario Balotelli amepigwa marufuku mchezo mmoja, na kutozwa faini ya pauni 25,000 na kuamriwa…na narudia tena, kuamriwa kuhudhuria kozi ya elimu au mafunzo ya bada ya kutoa matamshi ya kibaguzi.

Balotelli tayari alikuwa amekubali mashtaka ya kukiuka sheria ya Shirikisho la Kandanda la Uingereza, inayohusiana na asili ya kuzaliwa, rangi, uraia au utaifa wala dini, na imani, baada ya kuweka kwenye mtandao wake wa Instagram picha ya katuni ya mchezo wa kompyuta wa Super Mario, ambayo ilijumuisha maneno yaliyosema “anaruka kama mtu mweusi na kukamata sarafu kama Myahudi“.

Hii ina maana Balotelli ataukosa mchuano muhimu wa hapo kesho wa Premier League kati ya Liverpool na Arsenal uwanjani Anfield baada ya kuamua kutokata rufaa.

Muitaliano huyo aliomba msamaha kwenye ukurasa wake a Twitter, akisema hakunuia kumchukiza yeyote, na kwamba ilikuwa picha ya mzaha tu.

Hmmm, lakini kwa kwei mbona tu ni Mario? Mbona isiwe ni mimi? Mwisho wa michezo kwa sasa, umekuwa nami Bruce Amani, kwa habari zaidi, fungua ukurasa wetu wa michezo, dw.de/kiswahili/michezo. Nitafute pia kwenye ukurasa wangu wa Twitter, anuani yangu ni AmaniBruce. Kwaheri.

Mwandishi. Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com