Mazingira ya Afrika - Tishio Kwa Pepo Iliyopotea | Noa Bongo | DW | 01.06.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Noa Bongo

Mazingira ya Afrika - Tishio Kwa Pepo Iliyopotea

Afrika inachangia kidogo katika kuchafua mazingira lakini imeathirika sana na mabadiliko ya hali ya hewa. "Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako" inaangalia uhusiano baina ya watu na mazingira.

default

Misitu inakatwa kwa ajili ya kilimo. Watu wanawinda wanyama na kuvua samaki kila inapowezekana. Miji kadhaa inaonekana kufunikwa na taka, kwa sababu ukusanyaji taka ni ghali sana kwa watu masikini, wanaoishi mijini. Na kitisho kingine kinakaribia, Waafrika wengi zaidi hivi sasa wanapendelea kuendesha magari na kuchangia katika utoaji unaoongezeka wa gesi zinazoharibu mazingira.

Mtindo wa dunia

Athari za mabadilko ya hali ya hewa tayari zinaonekana katika maeneo kadhaa katika bara hili. Majira ya mvua yanakuwa mafupi, nyuzi joto zinaongezeka na upatikanaji wa maji umepungua. Wakaazi wa maeneo hayo wanabeba mzigo wa mabadiliko. Hawawezi tena kulima mazao yao ya kawaida na wanakosa maji wanayoyahitaji kuweza kuishi. Zaidi ya hayo, maeneo chepe chepe na misitu yenye mimea ambayo ni adimu na aina kadhaa za wanyama zinapotea.

Kupata njia mpya

Pamoja na kuwaletea wasikiliaji wake ukweli wote juu ya mazingira na changamoto zinazokabili hali hiyo, "Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako" pia inatoa njia mpya. Mchezo wa redio unakuletea vijana wanne wa shule za elimu ya juu katika kiu yao ya kutaka kufahamu mazingira yao. Ni nafasi kubwa kwa wasikilizaji wake kuwafuatilia na kugundua mengi jinsi ya kuiokoa dunia wanayoishi.

"Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako" kinapatikana katika lugha sita, Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Kwa taarifa zaidi ama jinsi ya kusikiliza vipindi hivi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.dw-world.de/lbe. Kipindi hiki kinadhaminiwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa