Mayweather, Pacquiao wakutana ana kwa ana | Michezo | DW | 13.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Mayweather, Pacquiao wakutana ana kwa ana

Baada ya miaka mitano ya kujigamba, Floyd Mayweather Jr. na Manny Pacquaio walisimama ana kwa ana ili kuzindua rasmi pigano lao linalosubiriwa kwa hamu kubwa

Mabondia hao wawili walijitokeza mbele ya waandishi wa habari ili kuanza kulipigia debe pigano lao linalosubiriwa mnao Mei 2.

Hakuna bondia yeyote kati yao aliyejibu maswali kutoka kwa wanahabari waliofurika katika ukumbi wa Nokia Theatre mjini Los Angels, lakini kila mmoja alielezea matumaini makubwa kuhusu pigano hilo. Mmarekani Mayweather alisema "Mei 2, ni pigano la karne na litawahusu mabondia wawili bora zaidi wakishuka ulingoni. Pacquaio ni mmoja wa mabondia bora katika enzi hii. Kila kitu kina muda wake na nadhani hakuna mda mwingine ambao tungeweza kuchagua. Mkakati wetu ni kuwa werevu na kushiriki pigano moja baada ya jingine, kama yote 47.

Naye Pacquiao aliziangalia kamera na kusema "kwa mashabiki wa masumbwi nadhani ni pigano ulokuwa ukilisubiri tangu miaka mitano iliyopita. Pigano lipo na sote tutafanya mazoezi makali kwa ajili ya pigano hili na kujitahidi mnamo Mei 2 kukufurahisha.

Pigano hilo litakaloandaliwa katika Ukumbi wa MGM Grand Garden Arena mjini Las Vegas linatarajiwa kuwa ndilo kubwa zaidi kimapato katika historia ya ndondi. Mayweather ameshinda mapigano 47 miongoni mwa hayo 26 kwa njia ya knockout, na hajashindwa pigano lolote. Pacquiao ameshiriki mapigano 57, kushindwa mara tano na kutoka sare mara mbili. Ameshinda 38 kwa njia ya knock out.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri:Gakuba Daniel

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com